Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

9 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

huku na hatupaswi kupuuzia ukweli huo. Hata hivyo, kuna uwezekano wa kupata msingi wa pamoja katikati ya tofauti hizo.

B. Msingi wa pamoja: kuunganishwa na Kristo na Kanisa lake kupitia huduma ya Roho.

1. Maandiko yanatufundisha kwamba tunampokea Roho Mtakatifu pale tu tunapookoka, na kwamba anatuunganisha na Kristo na Kanisa lake kwa njia ambayo, sio tu inatupatia haki ya kuwa sehemu ya Kanisa (kama vile kitendo cha kuasili kinavyoonyesha wazi), lakini pia tunashiriki nguvu iliyo hai na uwepo wa Kristo na watu wake kwa sababu tunashiriki nao katika ushirika huu na Roho Mtakatifu.

2. 1 Wakorintho 12:13

3

3. KUMBUKA: Ingawa si kila mapokeo ya kitheolojia yanatafsiri kipengele hiki cha kazi ya Roho kama “ubatizo katika Roho Mtakatifu” (wengine wanapendelea kuuita “kuzaliwa kwa Roho”), wote wanakubali kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kutuunganisha na Yesu na Mwili wake na kuwa nguvu hai na uwepo wa Kristo katika maisha yetu. Bila kujali tunaliitaje tendo hili, hili ni eneo muhimu la makubaliano ya Kikristo. C. Maeneo ya kutokukubaliana kuhusu ubatizo wa Roho: maswali ya msingi Kwa wakristo wengi ufafanuzi huo hapo juu (kuungamanishwa na Kristo na Kanisa lake) unamaanisha kwamba “kubatizwa katika Roho Mtakatifu” ni jambo linalotokea kwa kila mkristo pale tu anapookoka. Hata hivyo, wakristo wengi wanaamini kwamba kuna mistari fulani ya Biblia inayoweza kuibua maswali mengine kuhusu ubatizo wa Roho. Wanauliza: “Je, tunapokea yote ambayo Roho Mtakatifu anayo kwa ajili yetu pale tu tunapookoka au kuna ujazo mkubwa zaidi wa Roho Mtakatifu ambao huja baadaye tunapoendelea kuishi maisha ya Kikristo?” “Ikiwa ni hivyo, ujazo huu kamili unapokelewaje, ni ushahidi gani unaonyesha kwamba umetokea, na lengo la ujazo huu ni nini?”

Made with FlippingBook - Share PDF online