The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
1 1 4 /
UFALME WA MUNGU
c. Yesu hatatuma wawakilishi, wabadala, au wajumbe mahali pake wakati wa kukamilisha Ufalme wa Mungu ufikapo. Atakuja mwenyewe, binafsi.
2. Kuja kwake kutakuwa katika mwili .
a. Kuja kwake kutakuwa katika mwili, halisi, si kiroho au kiakili, Mdo 1:11.
b. Ujio wa kibinafsi utakuwa katika mwili ule ule ambao alipaa nao mbinguni.
3. Kuja kwake kutaonekana .
a. Yesu anasema kuja kwake kutaonekana mawinguni, na kwamba mataifa yataomboleza yatakapomwona akija juu ya mawingu ya anga, pamoja na nguvu na utukufu mkuu, Mt. 24:30.
4
b. Kuja kwa Kristo kutaonekana kwa macho ya wale wote watakaokuwa hai duniani.
4. Kuja kwake kutajawa na fahari na utukufu .
a. Ujio huo unafafanuliwa katika Injili za Zinoptiki (Injili ndugu) kama Bwana wetu Yesu akija juu ya mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu, Mt. 24:30; Marko 13:26; Luka 21:27.
b. Utatangazwa kwa mlio wa tarumbeta ya malaika mkuu, 1 Thes. 4:16.
Made with FlippingBook Learn more on our blog