The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 1 1 5

UFALME WA MUNGU

c. Utaambatana na uwepo wa malaika, Mt. 24:31.

d. Utahusishwa na Kristo Yesu kuchukua mamlaka yake ya kifalme kwenye kiti chake cha enzi, akihukumu na kutawala juu ya mataifa, Mt. 25:31-46.

5. Kuja kwake kutakuwa kwa ghafla na pasipo kutarajiwa .

a. Litakuwa tendo la kuja upesi, kama mwivi usiku, na wengi wakiwa hawajui kabisa kuhusu kurudi kwake, 1 Thes. 5:1.

b. Mfano wa wanawali kumi katika Mathayo 25 unadokeza ukweli huu.

c. Petro anaeleza kwamba kuchelewa kwa ujio wa pili wa Kristo kunaweza kusababisha wengine kudhihaki, lakini ahadi hiyo ni hakika, 2 Pet. 3:3-4.

4

d. Yesu anasema kwamba litakuja tendo la mshangao kama katika siku za Nuhu, na wakati wa Lutu – upesi, bila kutarajia, na kwa mshangao mkubwa, Luka 17:26-30.

6. Kuja kwake kutakuwa ni tukio la pamoja .

a. Waamini wengine wanaamini katika ujio wa awamu mbili (moja kwa siri “kwa ajili ya watakatifu,” na awamu ya pili hadharani, baada ya kipindi cha dhiki cha miaka saba, “kuja pamoja na watakatifu”).

Made with FlippingBook Learn more on our blog