The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
1 2 2 /
UFALME WA MUNGU
B. Ufufuo ni kazi ya Mungu wa Utatu, Bwana (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) . Kila mshiriki wa utatu anahusishwa moja kwa moja na ufufuo.
1. Baba kwa njia ya Roho, Rum. 8:11.
2. Yesu Kristo kama mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, Kol. 1:18.
C. Ufufuo ni ufufuo halisi, kufufuka kwa wafu katika mwili .
1. Rum. 8:11.
2. 1 Wakorintho 15:20 na kuendelea inazungumzia uhakika wa ufufuo wa kimwili kutoka kwa wafu, ufufuo wa Yesu ukiwa ni kielelezo cha ufufuo wa wote watakaokuja.
4
D. Ufufuo utakuwa ufufuo wa wote wenye haki na wasio haki.
1. Kufufuliwa kwa wenye haki:
a. Kunaelezwa mara nyingi kuwa wa uhakika.
b. Kuhusiana na thawabu, Isa. 26:9; Luka 14:14; Fil. 3:11.
2. Kufufuliwa kwa wasioamini:
a. Kunahusishwa na aibu na fedheha ya milele, Dan. 12:2.
Made with FlippingBook Learn more on our blog