The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
1 2 6 /
UFALME WA MUNGU
V. Hatima ya mwisho ya Kukamilishwa kwa Ufalme itakuwa Enzi Kuu ya Mungu: Mungu Atakuwa Yote-katika-Yote.
ukurasa 354 14
A. Utimilifu wa Ufalme utaakisi ujuzi wa Mungu kwa ulimwengu wote.
1. Kwa mara ya kwanza, sote tutamwona Mungu na kumjua Mungu kwa njia ya moja kwa moja, bila kuzingirwa na dhambi au uovu, Isa. 11:1-9.
2. Tutakuwa kama Yeye, kwa maana tutamwona jinsi alivyo, 1 Yohana 3:2.
B. Utimilifu wa Ufalme utasababisha kuondolewa kwa uovu wote, ambao utaondolewa na kuwekwa chini, chini ya miguu ya Yesu Kristo.
1. Viumbe vyote vitarejeshwa kwenye utukufu wake wa Edeni, Isa. 11:1-9.
4
2. Mateso yote, maovu, dhiki, na dhambi zitatoweshwa, pamoja na madhara yake milele, Ufu. 21:4.
3. Hata chanzo cha majaribu na mabaya kitawekwa chini na kuondoshwa milele, Ufu. 20:10.
C. Utimilifu wa Ufalme utawafanya waliokombolewa kuwa milki ya pekee ya Bwana, wale ambao watakuwa mali ya Mungu pekee, walioitwa kumwabudu na kumtumikia Mungu na Mwana-Kondoo.
1. Katika Yerusalemu Mpya, mji wa Mungu utakaoshuka kwa wanadamu, Ufu. 21:1-4.
Made with FlippingBook Learn more on our blog