The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

1 3 4 /

UFALME WA MUNGU

Ikiwa una nia ya kufuatilia kwa kina baadhi ya mawazo kuhusu nyakati za mwisho, na masuala kama vile unyakuo na dhiki kuu, unaweza kujaribu vitabu hivi: Archer, Gleason L. Jr., Feinberg, Paul D. et al. Three Views on the Rapture: Pre, Mid, or Post Tribulational? Grand Rapids: Zondervan, 1984. Ladd, G. E. The Blessed Hope: A Biblical Study of the Second Advent and the Rapture . Grand Rapids: Eerdmans, 1956. Utawajibika sasa kutumia maarifa ya moduli hii katika vitendo kwa njia ambayo wewe na mkufunzi wako mtakubaliana. Maana za kurudi kwa Yesu ni nyingi na zenye utajiri mkubwa: fikiria njia zote ambazo mafundisho haya yanaweza kuathiri maisha yako ya ibada, maombi yako, mwitikio wako kwa viongozi wa kanisa lako na kwa marafiki, mtazamo wako kazini, n.k. La maana ni kwamba utafute kuhusianisha fundisho hili la Ufalme na maisha, kazi, na huduma yako. Kazi ya huduma kwa vitendo imewekwa kwa kusudi hili, na katika siku zinazofuata utakuwa na fursa ya kuwashirikisha wengine maarifa haya katika maisha halisi na mazingira halisi ya huduma. Omba kwamba Mungu akupe ufahamu wa njia zake unaposhirikisha wengine ufahamu wako kupitia kazi hii. Je, kuna masuala yoyote, watu, hali, au fursa zinazohitaji kuombewa kama matokeo ya kujifunza kwako somo hili? Je, ni masuala gani hasa au watu ambao Mungu ameweka katika moyo wako ambao wanahitaji dua na maombi yenye malengo kuhusiana na somo hili? Chukua muda wa kutafakari hili, na upokee usaidizi unaohitajika katika ushauri na maombi kwa ajili ya yale ambayo Roho Mtakatifu amekuonyesha.

Nyenzo na Bibliografia

Kuhusianisha Somo na Huduma

4

Ushauri na Maombi

MAZOEZI

Hakuna kazi ya kukabidhi.

Kukariri Maandiko

Hakuna kazi ya kukabidhi.

Kazi ya Usomaji

Kufikia sasa, unapaswa kuwa umeainisha na kufanyia maamuzi mapendekezo yako kuhusiana na Kazi ya Huduma na Kazi ya Eksejesia na kuyakabidhi kwa Mkufunzi wako ili ayapitie na kuyapitisha rasmi. Hakikisha kwamba unapangilia shughuli zako vizuri mapema, ili usichelewe kukabidhi kazi zao.

Kazi Nyinginezo

ukurasa 356  17

Made with FlippingBook Learn more on our blog