The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 0 9

UFALME WA MUNGU

Biblia imejaa matamko ya kwamba Mungu wa mbinguni ni Mwenye Enzi Kuu, Bwana kamili wa vitu vyote, anayetawala kutoka juu kwa utukufu wake mwenyewe. “Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote” (Zab. 103:19). Yeye ndiye Mungu ambaye “anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye” (Dan. 4:17, 25, 34; 5:21; 7:14). Daudi anadokeza kwamba Mungu wa Maandiko anastahili uweza, utukufu, ukuu, na fahari kwa ajili ya kile alichoumba mbinguni na duniani (1 Nya. 29:11), jambo ambalo Yesu anarejelea katika sala yake (Mt. 6:13). Tangu mwanzo, Maandiko yanasema kwamba Bwana Mungu ndiye “Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana” (1 Tim. 6:15; taz. Ufu. 19:16). Unapoingia katika sehemu hii ya kwanza unapaswa pia kutambua kwamba majina ya Mungu yote yanaashiria na kudhihirisha ukuu wake kamili juu ya vyote ambavyo ameviumba. Yeye ni “Mungu Aliye Juu Sana” ( elyon , Mwa. 14:18-20), “Mungu Mwenyezi” ( el sadday , 17:1; rej. Kut. 6:2), “Bwana Mungu Mwenyezi” ( adonay yhwh , Mwa. 15:2; Kum. 3:24, NEN), na “Bwana Mungu Mwenye Nguvu” ( kyrios pantokrator , Uf. 1:8, BHN). Katika mambo yote Mungu anaonyeshwa kama Bwana, sio kama mtu anayeweza kupingwa au kukataliwa kwa urahisi. Dhana ya Mungu kujitegemea mwenyewe katika uwepo wake ni dhana muhimu inayohusiana na ukuu wake. Utawala wa Mungu umejikita katika asili yake, uwepo wake mwenyewe kama mwenye uwezo wote, aliye kila mahali, na Bwana wa yote. Tazama Kutoka 6:3 na Zaburi 104:24-30 kwa maandiko mengine juu ya namna anavyoutegemeza uumbaji wake, japokuwa hauhitaji uumbaji ili kuishi (taz. Zab. 50:7-12). Haki ya Mungu ya kutawala pia inatokana na uhakika wa kwamba vitu vyote ni vyake. Akiwa Muumba na Mfinyanzi wa vitu vyote, Mungu anaweza kufanya katika ulimwengu mzima lolote linalompendeza jinsi anavyoona inafaa. Hafungwi na sheria au mapenzi yoyote ya nje yake isipokuwa nafsi yake mwenyewe, na vitu vyote kila mahali ni vyake peke yake. Ukweli huu kuhusu Mungu wa Utatu unaweka msingi wa kumwelewa kama Bwana wa vyote (ona Zab. 103:19).

 7 Ukurasa 18 Kipengele I

 8 Ukurasa 18 Kipengele I-B

Made with FlippingBook Learn more on our blog