The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 1 0 /

UFALME WA MUNGU

Hadithi ya Ufalme haianzii na wanaume na wanawake, au hata kwa malaika na Lusifa. Utawala wa Mungu unaanza na nafsi yake, Yeye kama Mweza wa yote na Mkuu, Aliyeinuliwa juu ya viumbe na vitu vyote. Theolojia inayopaswa kuthibitishwa hapa ni ile inayoakisi ukuu na utukufu wa Mungu kama Aliyeinuliwa juu ya vyote, kama Asiye na kasoro yoyote, ambaye ubora wake haupimiki na unapita viwango vyote, ambaye lazima ajishushe ili kutazama mambo yaliyo mbinguni na duniani, ambaye ameweka utukufu wake juu ya mbingu (Zab. 8:1). Ingawa ni muhimu kwa kusudi la somo hili kusisitiza jinsi upinzani dhidi ya mapenzi ya Mungu Mwenye Enzi Kuu ulivyousukuma ulimwengu katika machafuko, ni lazima tuwe waangalifu tusihusishe nafsi ya Mungu na uharibifu huo. Ni lazima, hata tunapothibitisha uwepo wa upinzani dhidi ya utawala wake, kuthibitisha kwamba enzi kuu ya Mungu (ambayo inahusishwa na uwepo na utukufu wake) inadhihirishwa katika yote anayofanya, hasa katika mipango yake kwa ulimwengu na dunia yake. Kwa mfano, Mungu hufanya kila kitu kulingana na makusudi yake mwenyewe (Efe. 1:11), na utawala wake unahusishwa na mapenzi yake na nguvu zake (yaani aliumba kila kitu mbinguni na duniani), hakuna jambo lililogumu kwake (Yer. 32:17-23), kwa kuwa “yote yanawezekana kwa Mungu” (Mk. 10:27; 14:35; Luka 1:37). Anatawala juu ya mataifa (Mdo. 14:15-17; 17:24-28), na upinzani dhidi ya mapenzi ya Mungu ambao mnaelekea kuuangazia katika somo hili, ulifanyika ndani ya mipaka ya ufahamu na mpango wa Mungu mwenyewe (Mwa. 2:16-17), ikiwa ni pamoja na kifo na ushindi wa Yesu Kristo msalabani (Mdo. 2:23; 4:27 28). Somo hili, Kupingwa kwa Utawala wa Mungu , linaonyesha kile kilicho hatarini katika pambano la ufalme kati ya Mungu, Ibilisi, na wanadamu wanaochagua kupinga mapenzi yake. Zingatia hapa dhamira na makusudi ya shetani. Nia yake ni kumnyang’anya Mungu nafasi na ukamilifu wake, ili kujitwalia utukufu na sifa anazostahili Mungu pekee. Hiki ndicho kiini cha uovu, mwanzo wa uasi, na chimbuko la ulimwengu wa kipepo katika Maandiko, yaani, nia ya kumkaidi Mungu na kujitwalia utukufu ambao Mungu pekee ndiye anayestahili, ambaye kamwe hatagawana utukufu na sifa zake na mwingine (taz. Isa. 42:8).

 9 Ukurasa 19 Kipengele I-C

 10 Ukurasa 19 Kipengele II

Made with FlippingBook Learn more on our blog