The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 1 1

UFALME WA MUNGU

Jambo lililo wazi kutoka katika hadithi ya Mwanzo ni kwamba Mungu anawahukumu nyoka na wanadamu wawili wa kwanza, ambao wanaonyesha katika matendo yao aibu na hatia kwa dhambi yao. Hukumu ya dhamiri, kama hali ya mtu kujitambua mwenyewe kwamba amepinga utawala wa enzi kuu ya Mungu na kukiuka mapenzi yake mema, kwa hakika hutokea kupitia nguvu na uwezo wa Mungu wa Utatu: hukumu ya dhimiri hutoka kwa Baba (Ebr. 12:5), kutokana na kazi ya Mwana (Yuda 15; Ufu. 3:19), kupitia matendo ya Roho Mtakatifu 16. Leo, aina hii ya hisia ya ndani inakuja kupitia kazi ya Neno kama inavyotangazwa na mashahidi Wakristo, hasa wahubiri, ambao wameitwa kusema na kutangaza kwa ujasiri habari njema ya Ufalme wa Mungu katika Kristo (Mt. 18:15; Yoh. 16:7, 8; Efe. 5:11, 13; 1 Tim. 2:15). Kwa maana halisi, nguvu ya Neno la Mungu katika Sheria ni kuwatia hatiani wale ambao wamepinga utawala wa Mungu kwa kuwawezesha kuona kwa usahihi ni wapi, lini, na jinsi gani wamegeuka kutoka kwa neno jema la Mungu ili kutekeleza matendo yao wenyewe (Yakobo 2:9). Kwa maana moja, hadithi hii ya kutisha inajirudia kila mara mtu anapompinga Roho wa Mungu ili kujitahidi kwa namna yake mwenyewe kujitosheleza na kujitegemea. Maswali haya yameundwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa malengo muhimu na ukweli uliowasilishwa katika sehemu ya kwanza ya video. Utalazimika kupangilia muda wako vizuri, hasa ikiwa wanafunzi wako wamevutiwa na dhana fulani, na wanataka kujadili maana zake kwa kina zaidi. Ruhusu muda ufaao wa kuangazia mambo makuu, ili bado uwe na muda wa kutosha wa mapumziko kabla ya sehemu inayofuata ya video kuanza. Sehemu hii ya video inaangazia matokeo ya Anguka yenye sehemu tatu kwa maana ya athari zake kwa ulimwengu ( kosmos ), asili ya dhambi ya wanadamu ( sarx ), na kuachiliwa kwa shetani katika ulimwengu ( kakos ). Dhana hizi tatu zinahusiana katika Maandiko, na ingawa katika sehemu zimejadiliwa tofauti, itakuwa muhimu kwako kama mkufunzi kutengeneza miunganiko kati yazo. Kama matokeo mengi ya Anguko moja, tunapaswa kutarajia kwamba mambo haya matatu ya kweli yanatokana na chimbuko moja, kwa maana ya kwamba asili ya mambo hayo matatu ina mizizi yake katika jaribio la kupinga na kuhalifu utawala wa haki wa Mungu katika ulimwengu. Kadiri unavyoweza kuwasaidia wanafunzi wako

 11 Ukurasa 23 Hitimisho

 12 Ukurasa 23 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

 13 Ukurasa 24 Muhtasari wa Sehemu ya 2

Made with FlippingBook Learn more on our blog