The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 1 2 /

UFALME WA MUNGU

kuelewa miunganiko kati ya udunia, mwili, na shetani, ndivyo watakavyoweza kufikiria vyema zaidi kuhusu asili ya uovu duniani, na kukuza ufahamu wa hali ya juu wa asili ya kiroho ya matendo ya kutisha ambayo yamefanyika ulimwenguni tangu Anguko. Kile ambacho hatupaswi kufanya, hata hivyo, ni kujenga hisia au nadharia ya uwili ( dualism ), yaani kuna nguvu au falme mbili kinzani zinazolingana, ambapo ulimwengu wa uovu wa dunia uko katika vita dhidi ya enzi ya haki ya mbinguni, au ya Kanisa. Kama utakavyoona, uumbaji hauonekani katika suala la uovu; badala yake, ni nguvu iliyopangwa ya giza ambayo inaendesha na kutawala maisha ya mamilioni ya watu wasioijua wala kuamini katika neema ya wokovu ya Yesu Kristo. Kile ambacho Agano Jipya linafundisha kwa uwazi ni kwamba, kama matokeo ya Anguko, adui mkuu wa Mungu, Ibilisi, anatawala juu ya uwezo wa nia ya nafsi na nguvu za uovu katika ulimwengu wetu, ambaye kama mkuu wa nguvu hizi za giza za kiroho sasa anatekeleza mapenzi yake kwa namna yenye mipaka kama kichwa cha nguvu hizo, ambacho kinaonekana, kama mtu mmoja alivyosema, “kupangiliwa kwa kiwango cha hali ya juu na kwa ufanisi mkubwa” (Efe. 6:12). Ni wazi kwamba nguvu na mamlaka hizi zinatawala na kuyafanya mazingira na maisha ya wale wasiomjua Mungu kuwa ya utumwa (Efe. 2:1-2; Kol. 3:6). Maandiko yanafundisha kwamba, katika upinzani wake dhidi ya Mungu, shetani anatawala ufalme, ambao uko chini ya udhibiti wake (Mt. 4:8), na ambao unapinga kazi na wiwango vya utawala wa Mungu katika Yesu Kristo (Luka 11:18). Hakikisha kwamba wanafunzi hawachanganyi neno “ulimwengu” na maana ya “uumbaji.” Hazifanani, ingawa tafsiri yetu ya Biblia ya Kiswahili inaelekea kuzihusianisha kwa namna inayochanganya. Neno “ulimwengu,” linapotumiwa kuzungumzia uumbaji, hudokeza tufe ambalo Mungu aliumba kwa nguvu zake kuu, ulimwengu na vitu vyote, hai na visivyo hai ndani yake. Maana hii inahusiana na matokeo ya nguvu za uumbaji za Mungu. Neno “ulimwengu” (kama kosmos ) linahusiana na mfumo wa uovu usiomcha Mungu na wenye kutisha ambao unahuishwa na pupa, tamaa, na kiburi, ambao unapingana kwa kila njia na mapenzi ya Mungu na utawala wake, na ambao unaathiri mataifa na kuzuia maendeleo ya Ufalme wa Mungu. Hakikisha kwamba wanafunzi hawachanganyi neno “ulimwengu” kama uumbaji na neno “ulimwengu” ( kosmos ) kama mfumo na muundo wa uovu usiomcha Mungu duniani.

 14 Ukurasa 25 Kipengele I

Made with FlippingBook Learn more on our blog