The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 1 3

UFALME WA MUNGU

Enzi na mamlaka zinazojadiliwa hapa zinahusiana na mfumo wa mamlaka na uongozi wa mapepo na malaika walioanguka ambao Yesu aliushinda kwa kifo chake msalabani (taz. Kol. 2:15). Nguvu hizo na safu za upinzani za kimalaika ambazo zilimfuata shetani katika uasi wake dhidi ya Bwana Mungu sasa zimeshindwa kupitia kifo, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu ambaye alizifanya kuwa mkogo (onyesho) kupitia kifo chake msalabani. Vifungu vingi vinavyozungumzia enzi na mamlaka vinadokeza mamlaka ya kibinadamu (Rum. 13:1-3; Tito 3:1). Hata hivyo, matumizi ya kawaida ya kirai hiki kinachotumiwa na Paulo cha enzi ( archai ) na mamlaka ( exousai ) au nguvu ( dynameis ) yanaweka wazi kwamba anatumia maneno haya akizungumzia viumbe wenye akili wa ulimwengu wa roho, wa kimalaika; mara nyingi akiwataja kama nguvu za giza za roho/mapepo waovu (Rum. 8:38; 1 Kor. 15:24; Efe. 1:21; 3:10; 6:12; Kol. 1:16; 2:10; 2:15). Maneno mengine yanayotumika katika muktadha huu ni utawala au mamlaka ( kyriotetes , Efe. 1:21; Kol. 1:16), viti vya enzi (thronoi , Kol. 1:16), na watawala ( archontes ) wa dunia hii (1 Kor. 2:6). Kutokana na matumizi ya Paulo, inaonekana suala si kutupa picha ya kina ya uongozi wa uovu, bali ni kuthibitisha kwamba ulimwengu uko chini ya mamlaka hizi, jambo ambalo ni chukizo kwa Mungu, na linaalika hukumu fulani. Katika video hii, angalau athari nne kuu kuhusu asili ya dhambi zimetajwa. Suala la dhambi ya kibinafsi, asili ya dhambi, kuhesabiwa hatia na dhambi, na ukweli kuhusu kifo cha kimwili na cha kiroho vyote vinaunganishwa na dhana ya sarx iliyotolewa. Kilicho muhimu kwa wanafunzi kuona ni athari kamili ambayo Anguko lilikuwa nayo juu ya upotovu na dhambi ya wanadamu. Anguko la Adamu na Hawa lilikuwa na athari ya kutisha kihistoria kwa wanadamu wote, ambayo sasa imemwathiri kila mwanadamu. Kwa kuwa vizazi vyote vya wanadamu viliunganishwa kwa karibu sana na wazazi wale wawili wa kwanza wa kibinadamu, kutotii kwao na uasi wao vimechafua uzao wa jamii yote ya wanadamu, na sasa, kupitia matendo yetu wenyewe ya ukaidi na uasi, tunashiriki upya katika Anguko kupitia uchaguzi na maamuzi yetu ya dhambi.

 15 Ukurasa 25 Kipengele I-C

 16 Ukurasa 27 Kipengele II

Made with FlippingBook Learn more on our blog