The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 1 4 /
UFALME WA MUNGU
Katika majadiliano yajayo, wewe kama mkufunzi unapaswa kuzingatia umuhimu wa ukweli huu katika suala la Anguko, na mapambano yanayoendelea katika mzozo wa Ufalme. Kwa maana halisi, mzozo wa ufalme, ambao ndio msingi wa muundo wa Biblia kama ufunuo, na hadithi ya ufalme kama theolojia, ni pambano kati ya Mungu na Shetani, au tuseme, kati ya Shetani na Mpakwa Mafuta wa Mungu, Bwana Yesu Kristo. Yesu alidhihirishwa ulimwenguni ili kuziangusha na kuziharibu kazi za shetani (rej. Mwa. 3:15; 1 Yoh. 3:8; Ebr. 2:14; Kol. 1:13, n.k.). Hakikisha unaona kile ambacho mzungumzaji anazungumza kwamba kuachiliwa kwa Yule Mwovu ulimwenguni kunawakilisha matokeo mabaya zaidi ya Anguko, yenye uharibifu zaidi kuliko athari zingine zozote, na kwa sababu hivyo, hicho ndicho kiini cha dhamira na azimio la Mungu katika kurejesha utawala wake katika ulimwengu. Katika kuongoza mjadala huu, hakikisha kwamba wanafunzi wana uelewa sahihi juu ya athari za msingi ambazo Anguko lilisababisha juu ya ulimwengu, wanadamu, na shetani. Athari hizi ni vipengele muhimu katika tamthilia ya Ufalme wa Mungu, na, kwa mwanafunzi wa Maandiko, zinawakilisha nguzo tatu za maovu ambazo zinaweza kuwawezesha wanafunzi kuelewa asili ya uovu duniani, na kufunuliwa kwa uovu kihistoria, kulingana na ushawishi wake katika historia ya mwanadamu. Usisite kusisitiza kwa uwazi ukweli kuhusu kakos , kwani hii ndiyo athari kubwa zaidi ya athari na matokeo yote ya Anguko, na ndiyo ambayo Yesu aliizungumzia zaidi kuliko nyingine yoyote katika huduma yake duniani akipambana na watawala wa nguvu za giza. Zilizoorodheshwa katika sehemu hii ni kweli za msingi zilizoandikwa kwa muundo wa sentensi ambazo wanafunzi walipaswa kuwa wamezipokea kupitia somo hili, yaani, kwa njia ya video na majadiliano yako pamoja nao. Hakikisha kwamba dhana hizi zimefafanuliwa vizuri na zimewekewa mkazo kwa umakini mkubwa, kwasababu, kazi zao za majaribio na mitihani zitachukuliwa kutoka kwenye dhana hizo moja kwa moja.
17 Ukurasa 29 Kipengele III
18 Ukurasa 32 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
19 Ukurasa 33 Muhtasari wa Dhana Muhimu
Made with FlippingBook Learn more on our blog