The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 3 1 5
UFALME WA MUNGU
Katika kuwasaidia wanafunzi wako kutafakari mazingira yao wenyewe, unaweza kubuni maswali kadhaa ili kuchochea shauku na uzingativu wao. Kilicho muhimu hapa sio maswali yaliyoandikwa hapa chini, bali ni wewe na wanafunzi wako, kupitia mijadala, kutatua kada ya masuala, hofu, maswali, na mawazo ambayo yanatokana moja kwa moja na uzoefu wa maisha yao, na kuhusiana na maisha na huduma zao. Usisite kutumia muda mwingi kwenye swali fulani linaloweza kuibuka kutokana na mafundisho au mambo fulani maalum ambayo yanaendana hasa na muktadha wa huduma yao wakati huu. Lengo la sehemu hii ni wewe kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao wenyewe na mazingira ya huduma zao. Kwa mara nyingine tena, maswali yaliyopo hapa chini yametolewa kama miongozo na vitangulizi, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Chukua baadhi kati ya haya, au uje na yako mwenyewe. Jambo muhimu ni kwamba yaendane na muktadha wao wa sasa na maswali waliyo nayo. Mifano Halisi hii mitatu imetoa mkazo kuhusiana na uhusiano kati ya wazo la Mungu kuwa na mamlaka kama Bwana wa wote na uhalisia wa maumivu na uharibifu unaoshuhudiwa katika majiji na ulimwenguni. Bila shaka wanafunzi wako watakuwa wameshuhudia mambo ya kutisha katika maisha yao, katika maisha ya washirika wa makanisa yao, katika familia zao na kwa majirani, na katika ulimwengu wao. Ni lazima sasa waweze kutumia uelewa huu kupata tafsiri sahihi ya matendo hayo maovu na mambo ya kutisha, wakati huo huo, kuthibitisha kwamba Mungu Mwenyezi angali ni Bwana. Ingawa utawala na mamlaka ya Mungu vimepingwa, Yeye ni Bwana na Mfalme juu ya vyote, na anafanya mapenzi yake kupitia Kanisa na kwa njia ya Roho wake. Bila shaka, ni hadi Yesu atakapokuja katika utukufu, ndipo sala ya Bwana itakapofanyika kuwa kweli kikamili (yaani, mapenzi ya Mungu kufanyika duniani kama yanavyofanyika mbinguni). Hata hivyo, katika ulimwengu, ambapo bado tunavumilia dhiki na maumivu (Yohana 16:33), Yesu ameushinda ulimwengu (Yohana 12:9-11). Kuwasaidia wanafunzi wako kuishi na uhalisia wa Ufalme ambao ni “tayari/bado” ni sehemu muhimu ya moduli hii ya Capstone . Tumia Mifano Halisi kujadili ugumu wa ukweli huu, na wakati huo huo uwasaidie kujitahidi kujihusisha na jambo hili kwa urahisi, kwa kuzingatia taabu na masaibu yanayo wakumba watu mijini.
20 Ukurasa 34 Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi
21 Ukurasa 34 Mifano Halisi
Made with FlippingBook Learn more on our blog