The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 1 6 /
UFALME WA MUNGU
Dondoo hizi za vitabu zinafaa sana katika kueleza ukweli kwamba ingawa Mungu ndiye Bwana wa historia, kwa sababu ya Anguko, ulimwengu umelemewa kwa nguvu za uovu, na bado, Mungu kwa neema yake ameamua kuharibu uovu kwa njia ya Yesu Kristo, Mwanawe. Ukweli huu wa Anguko ni kitendo cha kwanza tu cha tamthilia ya ufalme, lakini ni muhimu, kwa kuwa kinatoa muktadha kwa wanafunzi wako kuelewa ni nini kiko hatarini katika mapambano ya utawala na umiliki katika ulimwengu. Kitabu cha Billheimer kinafaa sana katika suala hili. Ikiwa muda unaruhusu, tumieni muda pamoja katika maombi, mkimshukuru Mungu kwa ukuu wake na uweza wake, na azimio lake la kushinda mamlaka na nguvu ambazo zimeshindana na wanadamu tangu Anguko. Tumsifu Mungu kwa nafasi tuliyo nayo sisi wanaume na wanawake wa Kanisa, kuuwakilisha utawala wa Mungu mjini, na kumwomba Mungu ujasiri na uwezo wa kufanyika vyombo bora vya utawala wake na kutawala katika maeneno ambapo ametuweka. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa zoezi la wiki ijayo, hasa lile la kuandika muhtasari wa vitabu utakavyo waelekeza kusoma. Hili sio gumu; lengo ni kwamba wasome vitabu hivyo kwa kadiri wawezavyo na kuandika sentensi chache juu ya kile ambacho wanaamini waandishi walimaanisha. Huu ni ujuzi muhimu wa kiakili kwa wanafunzi wako kujifunza, kwa hivyo hakikisha kwamba unawatia moyo katika mchakato huu. Na kwa wale wanafunzi ambao wanaweza kuliona hili kuwa gumu, wahakikishie kuhusu dhamira ya zoezi hili, na uwasisitizie kwamba uelewa wao wa maelezo hayo ndio muhimu zaidi, si ujuzi wao wa kuandika. Ni kweli, tunataka kuboresha ujuzi wao, lakini si katika namna inayo dhoofisha lengo la kuwatia moyo na kuwajenga. Hata hivyo, hatutaki wafanye chini ya kiwango cha ubora wanachotakiwa kufanya. Jitahidi kutafuta mbinu zenye uwiano mzuri kati ya kuwapa changamoto ya kufanya kwa ubora na kuhakikisha hawavunjiki moyo.
22 Ukurasa 36 Nyenzo na Bibliografia
23 Ukurasa 36 Ushauri na Maombi
24 Ukurasa 37 Kazi
Made with FlippingBook Learn more on our blog