The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 2 0 /
UFALME WA MUNGU
wa Mungu kuwa “karibu” au “kukaribia” linadokeza kwamba kwa kuwapo kwa Yesu ulimwenguni, Ufalme umekuja.
Vipengele vyote vya Kujenga Daraja vya somo hili vinahusu kutambua mwanzo na/au kuanza kwa azimio la Mungu la kurejesha Ufalme wake duniani. Wazo la kuanza ni muhimu, sio tu kwa kutambulisha somo, lakini pia litakuwa muhimu kwa matumizi ya kweli za somo katika kipindi hiki. Kwa mfano, kujua kwamba hatua ya kwanza ya Mungu inao msingi katika kazi yake yote ya wokovu ni muhimu katika kutujengea mtazamo wa shukrani kwa Mungu, na pia kuwa na uhakika kwamba tunaamini kazi ya Ufalme ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mungu ndiye mfanyakazi, na sisi ni watenda kazi pamoja naye katika mavuno yake, kwa maana “sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu” (1Kor. 3:9). Mungu ndiye mwigizaji mkuu katika tamthilia ya wokovu, na jukumu letu ni kushiriki pamoja na Mungu kama watenda kazi pamoja katika shamba lake la mizabibu. Kiini hasa cha mifano hii ya kujenga daraja ni kusisitiza masuala ya wanafunzi, bila shaka, lakini kufanya hivyo kwa kuzingatia ukweli huu mkuu. Lengo la somo hili la pili ni utendaji wa Mungu katika historia kwa uhuru kama Mungu na mkuu kwa niaba ya ulimwengu wake aliouumba. Mungu, kwa sababu ya upendo na kujitoa kwake kwa ulimwengu wake, aliazimia kufanya kazi ya kurejesha utawala wa ufalme wake duniani. Azimio hili lililochochewa na upendo na neema yake, ndilo nguvu kuu, nia, na msukumo katika tamthilia ya ufalme. Kwa maneno mengine, licha ya kuhusika kwa wahusika wakuu na mataifa katika historia ya wokovu wa Mungu, kiini cha ukombozi kinatokana na moyo wa Mungu, azimio lake la kujiletea mabaki ya watu ambao wataishi milele katika ulimwengu mpya ambamo utukufu na sifa zake zitakuwa kuu. Katika kuelewa sehemu ya kwanza ya video, ni muhimu kuwa na dhana hii kama mandhari na mkutadha wa masuala yote na vipengee vyote vinavyoangaziwa. Hilo ni muhimu sana kwa faida ya uelewa kamili wa muujiza wa wokovu, yaani, kwamba katika uhuru wake, Mungu Mwenyezi, ambaye alikuwa amepuuzwa na kukataliwa, pamoja na kutotii kwa wanadamu wawili wa kwanza, aliazimia kuwarudisha chini ya utawala wake kwa ajili ya utukufu wake mwenyewe.
3 Ukurasa 43 Kujenga Daraja
4 Ukurasa 44
Muhtasari wa Sehemu ya 1
Made with FlippingBook Learn more on our blog