The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 2 1

UFALME WA MUNGU

Kuna masuala magumu yanayojitokeza katika mjadala wa uhuru wa Mungu na uasi wa shetani na wa Adamu na Hawa. Katika somo hili, ni muhimu kusisitiza kwamba Bwana Mungu alidumisha ukuu wake juu ya kila kitu katika ulimwengu, juu ya kila kitu alichokifanya, ingawa utawala wake ulipingwa na uumbaji wake. Mungu kamwe hakuachia au kusalimisha udhibiti wake kamili wa matukio kwa mamlaka au nguvu nyingine yoyote. Hata katika kukabiliana na upinzani wa moja kwa moja kwa mapenzi yake, hakuna kitu kinachoweza kutokea bila ridhaa yake, hata ikiwa Yeye mwenyewe sio sababu kuu ya kila tukio. Kwa kushangaza, ni vigumu kuelewa kwamba hili pia ni kweli kuhusu uovu, ambao hufanya kazi chini ya mipaka iliyowekwa na Mungu na kwa idhini yake. Uovu na uasi hauwezi kupita mipaka ambayo Mungu anaamua kuuwekea (Ayubu 1; 1 Kor. 10:13). Kwa hiyo, lazima uasi wa shetani na Anguko la Adamu na Hawa pia vitazamwe kama matendo yaliyoruhusiwa na Mungu kuwa sehemu ya kusudi lake la juu la ufalme, japokuwa, wahusika wenyewe waliwajibika kikamilifu kwa maamuzi na matendo yao kuhusiana na mapenzi ya Mungu. Hata hivyo, Mungu hawezi kulaumiwa kwa njia yoyote kwa kuupa uumbaji wake uhuru wa kutii au kutotii mapenzi yake. Kwa maana moja, ni muhimu kuelewa kwamba wazo la Mungu kama Shujaa ndicho kiini cha maono ya ufalme. Kwa kweli, kuna aina fulani ya asili takatifu inayohusishwa na vita katika Biblia wakati watu wa Mungu wanapokabiliana na adui za Mungu kwa nguvu za Mungu kwa kusudi la Mungu. Kwa mfano, kuna ibada na desturi za kidini zinazohusiana na vita vitakatifu, ambavyo Bwana ndiye Shujaa mkuu. Baadhi ya vitu hivi vilifanywa kabla ya vita. Wanajeshi wa Israeli walitakiwa kufanya matayarisho ya kupigana katika vita ambayo Yehova alianzisha. Katika baadhi ya mazingira yasiyo ya kawaida sana, kama vile katika vita vya Yeriko, wapiganaji walitahiriwa, jambo ambalo si jambo la busara kufanya kabla ya kuingia vitani (Yos. 5; taz. Mwa. 34)! Kuna baadhi ya ushahidi unaoonyesha kwamba kila mara walipotaka kupigana vita katika jina la Yehova vita hivyo vilitanguliwa na aina fulani ya dhabihu za kiibada, jambo ambalo linaonyesha kuwa mapigano yalikuwa zaidi ya operesheni ya kijeshi tu. Ufalme wa Mungu kimsingi ni vita; Mungu akifanya vita dhidi ya majeshi yaliyoasi mapenzi yake makuu, na dhidi ya wale wanaopinga mapenzi yake leo (kama vile 1 Sam. 13:1–15).

 5 Ukurasa 44 Kipengele I

Made with FlippingBook Learn more on our blog