The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 2 2 /
UFALME WA MUNGU
Azimio la Mungu la kusimamisha upya Ufalme wake katika historia ya wanadamu linaonekana katika usemi unaorudiwa mara kwa mara wa Agano la Kale: “Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” (rej. Yer. 11:4; 24:7; 30:22; 32:38; Eze. 8:8; nk). Nukuu hizi zinafunua ukweli kwamba Mungu, kupitia ahadi zake za agano kwa Ibrahimu na watu wake, amekuja kwa nguvu zote na utayari wote kwa viumbe vyake bila kujibakiza ili kupigana na adui zake na kufanya kazi kupitia watu wake ambao ni “hazina yake ya pekee” ( segulla , Kut. 19:5; Kum. 7:6; 14:2; 26:18; Zab. 135:4; Mal. 3). Kumiliki huku kwa watu wake, ni kwa ajili ya mataifa, ambayo Mungu alikuwa ameazimia kuwaletea wokovu kupitia Mzao wa Abramu. Kilicho muhimu hapa katika kuelewa nia ya Mungu ni uhusiano kati ya mapenzi yake makuu na nia yake ya neema, upendo, na fadhili, au, kama Biblia inavyoliweka, “fadhili zenye upendo” za Mungu au “upendo wa agano” ( hesed ), neno ambalo ( berit ) mara nyingi huhusishwa nalo (rej. Kum. 7:9; 1 Fal. 8:923; Dan. 9:4). (Mfano mmoja wa kuvutia wa hili unapatikana katika 1 Sam. 20:8, ambapo hesed inahusishwa na Yonathani anapoingia katika uhusiano wa kiagano na Daudi). Si tu kwamba hii ni picha ya wazi ya azimio la Bwana kukomboa na kubadilisha ulimwengu ili kuurudisha kwenye mfumo wake wa serikali kama awali, lakini pia inaonyesha jinsi Mungu anavyofanya kazi kutokana na upendo huu mkuu, fadhili zenye upendo ambazo huchochea matendo yake kwa niaba ya wale wanaohitaji neema yake. “Israeli” ndilo jina ambalo malaika alimpa Yakobo baada ya pambano lake katika maombi ya usiku kucha na malaika huko Penueli, ambalo limerekodiwa katika Mwanzo 32:28. Jina hilo lilitolewa kutokana na muktadha wa pambano hilo, kwa sababu Yakobo alishindana na Mungu na kwa njia fulani akashinda, alipewa jina hilo kwa sababu “kama mkuu, alipambana na Mungu na akashinda.” Jina hili, Israeli, ni jina la jumla walilopewa wazao wa Yakobo, ambaye yeye mwenyewe alikuwa mjukuu wa Ibrahimu, ambaye Mungu alimpa Ahadi, Ahadi ile ile ambayo ilifanywa upya kwa Isaka na Yakobo. Kwa hiyo, watu wa Mungu, watu wa agano waliowakilishwa na watu wote wa makabila kumi na mawili wanaitwa “Waisraeli,” “wana wa Israeli” (Yos. 3:17; 7:25; Amu. 8:27; Yer. 3:21), na “nyumba ya Israeli” (Kut. 16:31; 40:38). Kilicho muhimu kuona ni ukoo wa Ibrahimu, na kufanywa upya kwa Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na kwa uzao wake, ambao uliwakilishwa kihistoria na watu
6 Ukurasa 47 Kipengele II
7 Ukurasa 49 Kipengele III
Made with FlippingBook Learn more on our blog