The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 3 2 3
UFALME WA MUNGU
wa Israeli. Katika Agano la Kale, jina hili linatumika kwa njia tofauti. Kwa mfano, baada ya kifo cha Sauli, makabila kumi ya Kaskazini yalijitwalia yenyewe jina la “Israeli”, kana kwamba wao wenyewe waliwakilisha taifa zima (ona 2 Sam. 2:9, 10, 17, 28; 3:10, 17; 19:40-43). Taifa hilo lilipoendelea kukua, baada ya kugawanywa kwa ufalme baada ya Mfalme Sulemani, watawala na wafalme wa yale makabila kumi ya Kaskazini waliitwa “wafalme wa Israeli,” huku wafalme wa yale makabila mawili ya Kusini (Benyamini na Yuda) wakiitwa “wafalme wa Yuda.” Baada ya falme zote mbili za Kaskazini na Kusini kupelekwa utumwani na Ashuru na Babiloni mtawalia, jina “Israeli” lilianza kutumiwa tena kuwakilisha taifa zima kama wazao wa Abramu. Tukitazamia kwa hamu wakati ambapo, chini ya utawala wa Mungu, watu wa Mungu wa nyakati zote watakusanyika chini ya utawala wa Mungu katika Ufalme uliokamilika, tunaona kwamba neno “Israeli” limehusishwa na kundi hili, yaani, “Israeli wa Kweli” (Zab. 73:1; Isa. 45:17; 49:3; Yoh. 1:47; Rum. 9:6; 11:26). Kinachopaswa kutiliwa mkazo hapa ni mwendelezo wa kihistoria wa ahadi ya Mungu kwa wazao wa Abramu kama watu ambao kupitia kwao Masihi, au Mzao, angekuja, yule ambaye angeiokoa Israeli na kupitia kwake, mataifa. Katika maswali haya, utaona lengo ni kupata uelewa wa kina wa maudhui na kweli zinazo husishwa na mafafanuzi yaliyotolewa katika sehemu ya kwanza ya video. Zingatia kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa majibu kulingana na malengo ya somo la sehemu ya kwanza, hasa kujitoa kwa Mungu kama Shujaa, na uaminifu wake kwa agano lake ulioonyeshwa kupitia Ibrahimu, Israeli, Yuda, na Daudi. Hakikisha kwamba unazingatia muda hapa, ili kushughulikia maswali yaliyo hapa chini na yale yaliyoulizwa na wanafunzi wako, na uwe makini na mambo yoyote ambayo yanaweza kukuondoa kwenye uzingativu wa kweli muhimu na mambo makuu ya somo.
8 Ukurasa 51 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Sehemu hii ya pili inakazia kutimizwa kwa ujio wa Ufalme katika Yesu wa Nazareti. Kwa kweli, Yesu ndiye Mfalme ambaye nafsi yake ndiyo msingi wa mamlaka yake. Kwa maneno mengine, utambulisho wa Yesu ndio msingi wa Ukuu na mamlaka yake. Katika maisha na huduma yake, Yesu wa Nazareti anatekeleza jukumu la
9 Ukurasa 52 Muhtasari wa Sehemu ya 2
Made with FlippingBook Learn more on our blog