The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 2 4 /

UFALME WA MUNGU

Mfalme wa Yahweh, akiwaita watu kutoka katika ulimwengu ili wawe milki yake ya pekee (Isa. 55:5; Yoh. 10:16, 27). Akiwa Bwana na Mfalme, Yesu amewapa watu wake hukumu na viwango vyake ambavyo vinapaswa kudhibiti utendaji na matendo ya watu wake katika kila njia wanayojitawala ( 1Kor. 5:4-5; 12:28; Efe. 4:11-12; Mt. 28:19-20; 18:17-18; 1 Tim. 5:20; Tit. 3:10). Ni uweza na mamlaka yake ya kifalme ambayo kwayo yeye hulinda, kutegemeza, na kuhifadhi watu wake katikati ya dhiki, migogoro, na majaribu yao kwa ajili ya jina lake (2 Kor. 12:9-10; Rum. 8:35-39), na kupitia mamlaka yake ya kifalme aliyopokea kutoka kwa Baba yake, yeye kama Bwana hushinda na kuzuia ushawishi na athari za maadui zake, akielekeza nguvu zake kupambana nao (Mdo 12:17; 18:9-10; 1 Kor. 15:25). Kama aliyeteuliwa na Mungu kuwa na mamlaka yote mbinguni na duniani, anaamuru na kupanga vitu vyote viwepo kwa ajili ya utukufu na heshima yake kuu zaidi, na huamua wema wa asili katika mambo yote (Rum. 8:28; 14:11; Kol. 1:18; Mt. 28:19 20). Na kama Mwamuzi, siku moja atatekeleza hukumu ya haki ya Baba juu ya wale wote wanaokataa habari njema ya Ufalme, na yeye mwenyewe atalipiza kisasi juu ya wale wanaokataa utawala wake na kuasi Injili yake (Zab. 2:9; 2 Thes. 1:8). Muhtasari huu wa msingi kuhusu Yesu kama Mfalme unaonyesha kweli ambazo zinaungwa mkono na mawazo yaliyo katika sehemu hii ya video. Kinachopaswa kusisitizwa ni kwamba kile ambacho kilikuwa ni ahadi tu na kivuli katika agano la Ibrahimu, sasa ndani ya Yesu wa Nazareti, kimekuwa kweli na halisi. Katika Yesu Kristo, Mungu amefunua utukufu na nguvu za Ufalme wake. Uwepo wake na nguvu zake sasa zimefunuliwa katika maisha na matendo ya Yesu. Kwa maana hiyo, kuwapo kwa Yesu ulimwenguni kunawakilisha aina ya pekee ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu, ya tofauti, iliyowasilishwa kwa kina zaidi, na inayoshughulikiwa kwa uthabiti zaidi kuliko taswira yoyote ya utawala wa Mungu iliyowahi kutolewa hapo awali. Yesu anawakilisha aina ya ufunuo wa mwisho wa Mungu kuhusiana na ujumbe wa ufalme, nguvu zake, na udhihirisho wake (Ebr. 1:1-4). Kuingia kwa Yesu ulimwenguni kunawakilisha kiwango kipya cha makali na umakini kwenye vita ya kiungu ya Bwana ya kurejesha utawala wake ulimwenguni. Kiuhalisia, Yesu wa Nazareti anazidisha makali ya vita vya Ufalme ulimwenguni kwa kuelekeza nguvu kubwa sana si dhidi ya dhambi na uovu wa wanadamu, bali dhidi ya nguvu ovu za yule Mwovu, na mamlaka na enzi katika ulimwengu wa roho. Yesu anaanzisha Ufalme kwa nguvu ya kweli dhidi ya ufalme wa shetani,

 10 Ukurasa 53 Kipengele I

Made with FlippingBook Learn more on our blog