The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 3 2 5
UFALME WA MUNGU
lakini hapigani vita kwa mkuki na upanga, bali kwa silaha za vita vya rohoni katika Roho Mtakatifu. Kwa mfano, Petro anapoamua kutumia upanga kumlinda Yesu, anamkemea na badala yake anakwenda msalabani, ambayo ndiyo silaha kuu ya siri ya Ufalme wa Mungu (Mt. 26:50-56). Dhana hii ya Yesu kama Shujaa Mkuu na kifo cha Kristo msalabani kama silaha kuu inaelezewa na Paulo katika Wakolosai ambapo anazungumza juu ya kifo cha Yesu kama kunyang’anya enzi na mamlaka (Kol. 2:15), na kushindwa kabisa kwa enzi na mamlaka hizo kupitia msalaba. Kifo na kupaa kwa Yesu vinachukuliwa kama aina ya sherehe ya ushindi, gwaride la Jenerali Mkuu ambaye ameleta nyara na wafungwa wa vita katika gari-moshi la Mshindi wake hodari. Wazo hili linaweza kuonekana pia katika Waefeso 4:7-8, pamoja na nukuu yake kutoka Zaburi 68, wimbo wa kawaida wa vita vya kiungu. Katika namna ya ajabu, Bwana wetu Yesu aliwashinda maadui wa Mungu na kuzindua Ufalme, akishinda vita kubwa kuliko zote msalabani, kwa kuuawa, si kwa kuwaua wengine kimwili. Kwa namna fulani Yesu anaweka katika kuja kwake kielelezo na kiwango cha vita vyote halali vya kiroho. Tunamshinda adui si kwa kuangamiza maisha ya wengine, bali kwa kutoa maisha yetu kwa ajili yao; tunashinda vita dhidi ya maadui wa Mungu si kwa kuua wanadamu, bali kwa kuishi kama dhabihu iliyo hai, inayokubalika kwa Mungu (Rum. 12:2; Yn. 12:25). Tunashinda si kwa uwezo wa bunduki, kisu na kombora, bali kwa Neno la Mungu na ngao ya imani (Efe. 6:10-18). Kitendo cha Yesu kumshinda adui kunathibitisha kwamba sehemu kubwa ya vita inahusika na mapambano yetu binafsi ya ndani dhidi ya uovu uliobaki ndani (Rum. 7:7-25; 2 Kor. 10:1-6). Wazo hili, la kwamba kupitia kuja kwa Yesu Kristo Ufalme ulifunuliwa wazi katika ulimwengu, ni ufunuo muhimu katika utimilifu wa ahadi ya kiagano ya Mungu ya kurudisha utawala wake duniani. Pamoja na Yesu tunapitia uzoefu wa enzi ya Kimasihi katika uhalisia wake, si tu kama wazo au tumaini au shauku, lakini katika ukweli halisi. G. E. Ladd anaweka hoja hii kwa uwazi anaposema: Yesu alitangaza kwamba Ahadi hii [Ahadi ya kuja kwa Ufalme] hakika ilikuwa inatimizwa. Huu sio Ufalme wa kimaono bali ni wokovu wa sasa. Yesu hakuwaahidi
11 Ukurasa 54 Kipengele I-D
Made with FlippingBook Learn more on our blog