The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 2 6 /

UFALME WA MUNGU

wasikilizaji wake hatima bora zaidi au kuwahakikishia kwamba wangeingia katika Ufalme hivi karibuni. Badala yake alitangaza kwa ujasiri kwamba Ufalme (Herrschaft, yaani utawala) wa Mungu ulikuwa umewajia. Kuwapo kwa Ufalme kulikuwa “tukio, tendo la neema la Mungu.” Ahadi hiyo ilitimizwa katika kazi ya Yesu: katika kuwatangazia maskini habari njema, kufunguliwa kwa wafungwa, kuwarudishia vipofu uwezo wa kuona, kuwafungua walioonewa. Hii haikuwa theolojia mpya au wazo jipya au ahadi mpya; lilikuwa ni tukio jipya katika historia. “Wanyonge wanasikia habari njema, milango ya gereza iko wazi, waliokandamizwa wanapumua hewa ya uhuru, wasafiri vipofu wanaona nuru, siku ya wokovu imefika.” ~ G. E. Ladd. The Presence of the Future . Grand Rapids: Eerdmans Publishing, 1974. uk. 111-112. Kwa kuzingatia yale yote ambayo Yesu wa Nazareti aliyatimiza kupitia kifo, ufufuo, na kupaa kwake, kazi yake kama Shujaa wa Kiungu katika kuanzisha Ufalme wa Mungu bado haijakamilika. Usomaji rahisi wa kitabu cha Ufunuo na sehemu nyingine za kinabii za Agano Jipya unadhihirisha kwamba atatimiza huduma aliyoianzisha katika maisha yake, kifo, ufufuo na kupaa kwake. Yesu mwenyewe alizungumza juu ya siku kuu ambayo yeye kama Mwana wa Adamu angekuja juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na malaika watakatifu ili hatimaye na kwa ukamilifu apate kuzishinda nguvu zote ambazo zingepinga mapenzi yake (Mk. 13:26). Maono haya na lugha hii vinaakisi maono makuu ya nabii Danieli, ambaye anamzungumzia mtu kama huyo katika Danieli 7:13. Ufalme wa Mungu unakuja kwa nguvu, kama vile Yohana Mbatizaji alivyotabiri ungekuja. Bwana wetu, ambaye alikuja mara ya kwanza kutekeleza silaha ya siri ya Mungu ya msalaba juu ya adui zake, kwa kweli atarudi tena, wakati huu akiwa Shujaa wa kweli wa Kiungu ambaye kazi yake ni ya wazi, kamilifu, na yenye uharibifu kwa adui zake. Ufunuo 19:11-16 inaeleza ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo katika taswira ya Shujaa wa Kiungu; anakuja juu ya farasi mweupe, aliyevikwa vazi liliyochovywa katika damu, na upanga wenye makali kuwili ukitoka kinywani mwake. Nyuma yake kuna majeshi kamili ya mbinguni “anapohukumu na kufanya vita” (mstari 11). Maono ya mwisho ya Biblia kuhusu Yesu kama Shujaa wa Kiungu wa Mungu yanamalizia ufunuo huo kwa taswira ya ajabu ya vita vya mwisho, ambavyo, kwa uchache sana, lazima viwe ishara toshelevu na yenye nguvu ya hukumu ya mwisho

 12 Ukurasa 61 Hitimisho

Made with FlippingBook Learn more on our blog