The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 2 7

UFALME WA MUNGU

na ya kisasi inayokuja na ghadhabu ya Mungu aitoayo kwa wale ambao wamepinga utawala wake bila kutubu. Katika uhalisia, Yesu wa Nazareti ndiye Mpakwa Mafuta, aliyechaguliwa na Mungu ili kukomesha pambano lililoanza na uasi wa nyoka na kutotii kwa wanadamu wawili wa kwanza. Ni yeye ambaye atamponda ponda kakos, yule ambaye kupitia uwongo na udanganyifu wake alileta taabu na mateso juu ya dunia (Rum. 16:20; Ufu. 12:9), na ambaye anawakilisha aina mbaya zaidi ya upinzani wa ukaidi kwa utawala wa Mungu. Ahadi ya Mwanzo 3:15 hatimaye imetimia katika nafsi ya Mnazareti mpole, anayefanya vita vya Mungu, si kwa kuua bali kwa kufa na kufufuka tena kwa niaba ya wale aliokuja kuwaokoa. Lengo la maswali haya katika kipengele hiki sio kukufanya uhisi hitaji la kulipitia kila moja. Sio tu kwamba hili litakuwa jambo gumu na la kuchosha, linaweza pia kukuondoa katika kuzingatia masuala mengi magumu na muhimu ya wanafunzi wako. Ingawa maswali haya yanakusudiwa kukusaidia kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa dhana zilizoonyeshwa kwenye video, itabidi uweke uwiano kati ya lengo hilo na lengo dhahiri la kushughulika na maswali na mambo yale wanayovutiwa nayo wanapoitikia Maandiko na nyenzo zingine. Mojawapo ya malengo katika kuangazia mifano halisi katika somo hili ni kufanya muunganisho maalum na muhimu wa yale mambo ya kieskatolojia ambayo bila shaka ni magumu sana na utendakazi wa vitendo wa huduma katika jiji. Mojawapo ya mambo yenye changamoto zaidi kwa wanafunzi kufanya ni kuona uwiano kati ya mafundisho ya maandiko juu ya Ufalme na maisha yao wenyewe na huduma. Iwapo unatumia au hutaki kutumia mfano halisi hapa chini au utachagua kubuni tukio lako mwenyewe la kujadili, lazima utafute kufanya muunganiko kuwa wazi kati ya kile ambacho wanafunzi wamesikia, kujifunza, na kujadili, na kile wanachokabiliwa nacho katika huduma zao. Kwa kuzingatia hili, mfano wa hapa chini unajaribu kuchukulia kwa uzito kile ambacho kingetokea ikiwa kunaweza kuwa na msisitizo usiofaa au uliotiwa chumvi juu ya Ufalme kama jambo lililopo tayari, au kama ungechukuliwa kuwa jambo la wakati ujao tu. Amini usiamini, jinsi mhudumu wa mijini anavyoitazama theolojia hii itakuwa na athari kubwa juu ya namna atakavyoiendea huduma na kuendelea katika kazi yake kwa ajili ya Bwana.

 13 Ukurasa 61 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

 14 Ukurasa 64 Mifano Halisi

Made with FlippingBook Learn more on our blog