The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 2 9

UFALME WA MUNGU

Uvamizi wa Utawala wa Mungu

MAELEZO YA MKUFUNZI 3

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa Somo la 3, Uvamizi wa Utawala wa Mungu . Lengo la jumla la moduli ya Ufalme wa Mungu ni kuwawezesha wanafunzi wako kufahamu nguvu, ajabu, na ukuu wa Ufalme wa Mungu, na maana yake kwa maisha na huduma zao katika makanisa wanamoabudu na kutumika. Jukumu la Kanisa, la kiulimwengu na la mtaa, ni kipaumbele cha mjadala huu, kwa kuwa Kanisa linatazamwa kama kituo na chombo ambacho kwacho ujumbe na nguvu za Ufalme zinadhihirishwa katika enzi hii. Somo hili limekusudiwa kuwaonyesha wanafunzi jinsi Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo, amelifanya Kanisa la Yesu Kristo mahali ambapo utukufu na uweza wa ufalme unadhihirishwa ili ulimwengu upate kuuona. Vile vile, Kanisa ni wakala, naibu wa Mungu katika kuwakilisha mamlaka na utawala wake ulimwenguni, na kutoa ushuhuda wa kweli na madhihirisho ya nguvu zake. Unachohitaji kufanya na wanafunzi katika somo hili ni kuwatia moyo kwa kuangazia tendo hili la ajabu la neema ya Mungu kulipatia Kanisa umuhimu na cheo kama hicho, na kusisitiza upendeleo wa ajabu walio nao kama Wakristo na wahudumu wa mijini kwamba Bwana amewapa fursa ya kulipenda na kulitumikia kanisa la mjini. Malengo haya yameelezwa kwa uwazi katika sehemu ya “Malengo ya Somo” na unapaswa kuyasisitiza katika somo lote na wakati wa majadiliano na muda wote uwapo na wanafunzi. Katika kila jambo mkazo umewekwa juu ya uwezo wa Kanisa wa kudhihirisha na kushuhudia uhalisia wa Ufalme. Kilicho muhimu hapa ni kwamba hili sio tu matokeo ya azimio na kujitoa kwa Kanisa. Kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, Kanisa sasa linaweza kuwa kundi ambalo kupitia hilo utawala wa Mungu unatambulishwa kwa wale ambao hawajui lolote kuhusu ushindi mkuu wa ufalme wa Mungu katika Kristo. Kwa maana halisi, hawatajua kamwe juu ya ushindi huo wa ufalme bila huduma ya uaminifu ya Kanisa kuonyesha ubora wa Bwana kwa njia ambayo itawalazimisha kuzingatia kazi ya Mungu katika Kristo (1 Pet. 2:9 10). Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo unavyoongeza uwezekano wa wao kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya. Ibada hii inaunganisha na kuhusianisha huduma ya Yesu kama Shujaa wa Kimungu na huduma inayoendelea ya Kanisa kama askari wa Mungu duniani wanaojivika ushindi wa Yesu na kuueneza ulimwenguni (Efe. 6:10-18). Yehova, kupitia uaminifu wake wa agano na ufunuo wa utukufu wake katika Mwanawe, amezindua utawala wake katika Yesu Kristo. Kama muumbaji na Mungu mkuu wa

 1 Ukurasa 69 Utangulizi wa Somo

 2 Ukurasa 69 Ibada

Made with FlippingBook Learn more on our blog