The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 3 0 /
UFALME WA MUNGU
ulimwengu, sasa ndani ya Yesu wa Nazareti anathibitisha tena waziwazi utawala wake juu ya mataifa yote (rej. Kum. 7:6). Vita vya Mungu katika Agano la Kale vilidhihirishwa kwa njia ya vita vitakatifu ambavyo alivianzisha kupitia watu wake dhidi ya adui zake. Kwa hivyo, vita vya kiroho na “jeuri” inayohusishwa navyo bila shaka ni kazi ambayo kwayo Shujaa wa Kimungu anatekeleza mapenzi na makusudi yake makuu katika ulimwengu. Bila shaka, katika enzi ya sasa hii ni aina ya unyanyasaji dhidi ya falme na mamlaka zinazopinga mapenzi ya Mungu na kuendesha mambo ya wale wasiomjua (k.m., Efe. 2:2; Kol. 3:5). Hata hivyo, hadithi ya Ufalme ni hadithi ya Mungu kufanya jeuri dhidi ya nguvu na mamlaka hizo ambazo zinapinga nia yake njema na haki yake halali ya kutawala kama Bwana na Mfalme juu ya wote. Kama ilivyotajwa hapo awali, kiini cha somo hili ni jukumu ambalo Mungu amelipa Kanisa la kutoa ushahidi na uthibitisho wa utawala wake duniani. Mifano halisi iliopo hapa chini imekusudiwa kufafanua kwa usahihi katika fahamu za wanafunzi uhusiano uliopo kati ya Kanisa na mtu anayekusudia kujitoa kwa Yesu. Ni jambo la kawaida sana katika siku zetu watu kudai kuwa na urafiki wa ndani na Yesu huku, wakati huohuo, wakilichukulia Kanisa kama kitu cha ziada kisicho na umuhimu mkubwa. Kwa hakika, wengi wanaodai kutembea kwa ukaribu na Kristo wanaamini wameweza kufanya hivyo kwa sababu ya kujiweka mbali na Kanisa. Kanisa linatazamwa, kama si sawa na adui, angalau kama kizuizi kikuu cha ukuaji na kina cha ufuasi wa Kikristo. Kwa kushangaza, mashirika mengi ya Kikristo yasiyofungamana na dhehebu na/au Kanisa lolote yanatoa hisia kwamba yenyewe ni kiungo cha Ufalme, na kwamba kanisa la mahali pamoja limekusudiwa kucheza kama mchezaji wa ziada katika timu ya Mungu. Somo hili linakabiliana na aina hiyo ya fikra. Kwa nguvu zaidi, linaita fikra kama hiyo kuwa ya uwongo, na labda, kutegemeana na kiwango cha kupotoka kwa fikra ya namna hiyo, tunaweza hata kusema ni uzushi. Lengo hapa ni kuwafanya wanafunzi kutafakari kwa pamoja kwa kuchunguza mifumo yao ya maisha binafsi na ya ushirika, ni uhusiano gani uliopo kati ya utii wao kwa Kanisa na ukiri wao wa kuwa na ukaribu na Kristo na kujitoa kikamilifu kwake. Somo litathibitisha kuwa huwezi kuwa na moja bila nyingine. Ili kueneza fikra za mwanakanisa mmoja mzuri wa karne ya nne, Padre wa Kilatini Cyprian, “Ikiwa Kanisa si mama yako, basi Mungu si Baba yako!”
3 Ukurasa 70 Kujenga Daraja
Made with FlippingBook Learn more on our blog