The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 3 1

UFALME WA MUNGU

Kusudi kuu katika sehemu hii na ile itakayokuja ni kuwasaidia wanafunzi wetu wakubali ushirika wa Kanisa na Ufalme kama utawala wa Mungu ulimwenguni. Neno “kanisa” huenda linatokana na neno la Kiyunani kuriakon linalomaanisha “nyumba ya Bwana.” Katika Agano Jipya, neno linalotafsiriwa kama “kanisa” mara nyingi ni tafsiri ya neno la Kiyunani ekklesia , “kusanyiko” au “walioitwa” (pengine ni sawa na qahal ya Kiebrania ya Agano la Kale). Ekklesia na qahal yote mawili yalitumika kubainisha, kwa matumizi rahisi, mkusanyiko au mkutano. Neno linalotumiwa katika Agano Jipya halikuhusishwa na mahali pa kukutania au jengo, wala kwa njia ya kawaida neno hilo halihusishwi na madhehebu (“Kanisa Huru la Kiinjili”) au watu wa nchi fulani wenye wito na malengo ya kufanya kazi moja (“Kanisa la Scotland”). Badala yake, neno hilo lilitumiwa kwa ajili ya: 1) kusanyiko au mkutano [Mdo 19:32, 39, 41]; 2) jamii nzima ya waamini wote waliomjia Mungu katika Kristo kwa toba na imani [k.m. Efe. 5:23-29; Ebr. 12:23]; 3) kusanyiko dogo la wanafunzi wanaokutana pamoja kwa ajili ya ushirika na utume [Rum. 16.5; Kol. 4:15]; 4) waamini katika mji au eneo fulani mahususi, kama “Kanisa la Mungu la Korintho” [1 Kor. 1:2, “Kanisa la Yerusalemu,” Mdo. 18:1, au “Kanisa la Efeso,” Ufu. 2:1]; 5) kundi zima la watu walio hai wanaokiri kuwa Wakristo wanaomwamini Kristo katika ulimwengu wa leo [1 Kor. 15:9; Gal. 1.13; Mt. 16:18]. Hii inarejelea “Kanisa linaloonekana,” yaani, waamini wanaokiri hadharani imani na tumaini lao katika Yesu Kristo katika ulimwengu wa leo. Kilicho muhimu kwako kama mkufunzi ni kujaribu kusisitiza katika mijadala na mazungumzo yako na wanafunzi kwamba Kanisa ni muhimu kwa makusudi ya ufalme wa Mungu, kwamba ingawa Ufalme wenyewe si Kanisa, kwa kweli ni kituo na muktadha wa Ufalme; mahali ambapo utawala wa Mungu unafurahiwa, unadhihirishwa, na kutolewa ushuhuda kupiti maisha, maneno, ibada na huduma. Lengo ni kuondoa mawazo yote ambayo Ufalme unaweza kueleweka katika maana yake halisi nje na/au kinyume na ufahamu muhimu na wa kibiblia wa Kanisa la Yesu Kristo ulimwenguni leo. Moja ya ukweli wa ajabu kuhusu Neno la Mungu kuhusiana na Kanisa ni wingi wa ajabu wa picha, mafumbo, mawazo, na dhana zinazohusiana na asili ya Kanisa la Yesu Kristo. Katika kitabu kizuri ajabu cha Paul Minear kuhusu Kanisa, Images of the Church in the New Testament , kiambatisho chake kinaorodhesha baadhi ya taswira tisini na sita alizozipata kwenye Kanisa, ambazo zimepewa uainishaji mbalimbali

 4 Ukurasa 72 Muhtasari wa Sehemu ya 1

 5 Ukurasa 72 Kipengele I

Made with FlippingBook Learn more on our blog