The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 3 2 /
UFALME WA MUNGU
kama picha ndogo, watu wa Mungu, uumbaji mpya, ushirika katika imani, na mwili wa Kristo. Anachopokea mtu katika kuutazama ufunuo katika Agano Jipya kuhusu Kanisa ni utajiri wa kina wa mawazo ya kitume katika kulitazama na kuliainisha Kanisa. Miongoni mwa yalioorodheshwa na Minear ni chumvi ya dunia, wapiganaji dhidi ya Shetani, watumwa waliotakaswa, marafiki, wana wa Mungu, nyumba ya Mungu, barua kutoka kwa Kristo, matawi ya Mzabibu, bibi mteule, bibi-arusi wa Kristo, wahamishwa, mabalozi, taifa teule, hekalu takatifu, ukuhani, uumbaji mpya, washirika pamoja na Kristo, na mwili wa kiroho. Orodha hiyo iliyojaa utajiri kama huo wa taswira inaonyesha kwamba Mitume hawakuhisi haja yoyote ya kuwekea mipaka ufafanuzi wa Kanisa kwa kushikilia taswira chache, au kufungia maana ya Kanisa katika kisanduku cha maana zilizomo katika Kanuni za Imani. Jukumu ambalo Kanisa linafanya ulimwenguni ni kamili na tofauti kama zilivyo taswira tofauti tofauti ambazo Yesu na Mitume walizitoa kuhusiana nalo. Kwa hakika, tunaweza kugundua utajiri mkubwa wa ufahamu wa aina mbalimbali kuhusu Kanisa kutokana na utafiti wa kina na wa kimakusudi wa taswira hizi na uhusiano uliopo baina yazo. Hata hivyo, katika Taasisi yetu, tumeona kuwa inasaidia kushikilia kwa uaminifu theolojia inayotokana na Kanuni ya Imani ya Nikea. Dhamira hii, imefanya kuwa muhimu kwetu kuelezea jukumu na asili ya Kanisa kupitia mafafanuzi ya kihistoria yaliyotolewa katika Kanuni ya Imani ya Nikea, yaani, kwamba Kanisa ni moja, takatifu, katoliki, na la kitume. Kwa msingi wa Mtaguso wa Konstantinopoli mwaka wa 381 B.K na kuthibitishwa tena huko Efeso (431) na Kalkedoni (451), Kanisa limejithibitisha kuwa “moja, takatifu, katoliki na la kitume.” Ingawa hatusemi kwa msisitizo wote kwamba hizi ndizo njia pekee za kuelewa asili ya Kanisa, tunashauri kwamba Wakristo katika historia nzima wameona aina hizi kuwa za msaada na za kuvutia katika kukusanya pamoja maarifa mbalimbali na yenye utajiri katika Agano Jipya juu ya Kanisa. Taswira ya mwili ni mojawapo ya sitiari zenye maana sana za Kanisa. Inatoa uelewa mzuri wa mahusiano ya viungo mbalimbali vya mwili kwa kila kimoja, pamoja na mifumo na miunganiko tofauti ya mwili. Agano Jipya bila shaka linasema kwamba Wakristo ni mwili mmoja katika Kristo unaojumuisha washirika wengi wanaohudumu katika ofisi, karama, na kazi mbalimbali kwa manufaa ya mwili wote (Rum. 12:4-5; 1Kor. 12:27). Kanisa limeteuliwa kuwa mwili wa kweli
6 Ukurasa 74 Kipengele I-C
Made with FlippingBook Learn more on our blog