The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 3 3 3
UFALME WA MUNGU
na mmoja wa Kristo ulimwenguni (Efe. 1:22-23; 4.12), na Yesu mwenyewe akiwa Kichwa (mamlaka na chanzo) cha mwili (Efe. 5:23; Kol. 1:18). Kama vile mwili unavyotegemea kichwa kabisa kwa maisha yake yote, ukuaji, mwelekeo, na utunzaji (Kol. 2:19), ndivyo Kanisa la Yesu Kristo lilivyoungamanishwa naye na kumtegemea. Ulinganisho wa mwili unaonyesha wazi jinsi ambavyo Kanisa ni zaidi ya kusanyiko la kawaida, badala yake ni mahali ambapo wale wanaoshiriki nasaba ya Kristo hukusanyika, kuhusiana, na kukua. Kanisa ni mahali ambapo Yesu anaweza kudhihirika duniani; kama mwili wake, Kanisa ni mfupa na nyama sawa na yule Shujaa wa Kimungu mwenyewe (kweli ambayo inathibitishwa tena katika sitiari ya Bibi-arusi katika Waefeso 5:22-33). Katika ufahamu wa kibiblia wa ndoa, mume na mke wanasemekana kuwa mwili mmoja, na ndivyo ilivyo kuhusu Kristo na Kanisa (Efe. 5:31-32). Mifano yote miwili zinazungumza kwa nguvu na moja kwa moja juu ya muungano wa hali ya juu ambao Yesu wa Nazareti anao na watu wake. Mantiki ya hili haiwezi kupingwa. Ikiwa Yesu ndiye Shujaa wa Pekee aliyezindua na kuuanzisha utawala wa Mungu kwa nguvu, na ikiwa Kanisa limeunganishwa naye kihalisi kwa imani, basi lazima kuwe na uhusiano wa moja kwa moja kati ya uwepo hai wa Kanisa na maisha na nguvu halisi za Ufalme. Popote palipo na Kanisa la kweli, lazima kuwe pia na uthibitisho na ishara ya uwepo, uhai, na nguvu za Ufalme. Pengine ishara kuu zaidi kwamba Kanisa ndicho kituo na wakala wa Ufalme katika enzi ya sasa ni ukweli kwamba Roho Mtakatifu anakaa ndani ya watu wa Mungu. Hakuna ushahidi mwingine wowote wa uwepo wa Ufalme ulio na uzito au wenye kauli ya mwisho kama huu, kama ilivyoelezwa katika ushuhuda wa Petro mwenyewe siku ya Pentekoste iliyorekodiwa katika Matendo 2. Katika Matendo 2:14 na kuendelea, Petro anaelezea matukio yenye nguvu ya ndimi katika siku ya Pentekoste kama ishara ya utimilifu wa unabii wa kitabu cha Yoeli kuhusu kuja kwa Roho Mtakatifu juu ya wote wenye mwili katika kipindi cha mwisho cha Kimasihi (taz. Yoeli 2:28-). Kama ishara ya uwepo wa Ufalme katika enzi ya Kimasihi, kumwagwa huku kwa Roho katika Kanisa kulikuwa ni ishara ya neema ya Mungu iliyotolewa kwa Wayahudi na Wamataifa kadhalika (Mdo. 10:45; 11:15). Kipawa hiki cha Roho, kinachohusishwa na ujio wa Shalom ya Mungu katika nyakati za mwisho, sasa kinaweza kupokelewa kwa toba rahisi na imani
7 Ukurasa 74 Kipengele II
Made with FlippingBook Learn more on our blog