The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 3 4 /
UFALME WA MUNGU
katika kazi ya wokovu ya Yesu wa Nazareti (Mdo. 2:38). Zawadi ya wokovu inayohusishwa na kuingia kwa Ufalme, kumiminwa kwa Roho Mtakatifu, sasa inapatikana kwa mtu yeyote, awe Myunani au Myahudi, baada ya kubatizwa katika Jina la Yesu Kristo, ahadi ambayo si kwa Wayahudi tu bali, kulingana na Petro, kwa yeyote na wote ambao Bwana Mungu anaweza kuwaita (Mdo. 2:39; Yoeli 2:32). Kanisa lilihuishwa tangu mwanzo na huduma ya Roho Mtakatifu, ambaye alichagua viongozi wao (Mdo. 13:1-3; Mdo 20), alitia nguvu huduma za viongozi wao (Mdo. 4:31; 6:5; 7:54; n.k.), na liongoza kazi endelevu za uenezi wa Injili na utume wa Kanisa ulimwenguni (Mdo. 9:31; 13:28; 15:28; 16:6-7). Kwa sababu ya uwepo wa Roho Mtakatifu katika Kanisa, matendo yale yale ya udhihirisho wa ufalme (uongofu, uponyaji, kutoa pepo, miujiza, n.k.) yalifanywa mara kwa mara katikati ya watu wa Mungu. Roho Mtakatifu mara kwa mara alitoa maono ya ufunuo na unabii kwa washirika wa Kanisa (Mdo. 9:10; 10:3; 10; 11:27-28; 13:1; 15:32) kama ilivyotabiriwa waziwazi katika unabii wa Yoeli 2. Kwa dalili zote za maisha na utume wa Kanisa, lilithibitisha katika maisha yake wa kila siku kwamba Ufalme wa Mungu, udhihirisho wa enzi ya Kimasihi ya Mungu, ulikuwa umekuja siku ya Pentekoste. Utawala na uwepo huu wa ufalme utakuwa pamoja na Kanisa hadi mwisho wa nyakati (Mt. 28:20). Katika maswali haya, utaona lengo ni kupata uelewa wa kina wa maudhui na kweli zinazo husishwa na mafafanuzi yaliyotolewa katika sehemu ya kwanza ya video. Ingawa mambo mengi yanaweza kuangaziwa katika sehemu hii, pengine jambo kuu la kuangaliwa upya ni jinsi Kanisa la Yesu Kristo lilivyoungamanishwa kihalisi na Kristo kupitia Roho Mtakatifu. Tena, Roho Mtakatifu katikati ya Kanisa ni ushahidi usiopingika kwamba Mitume walielewa kwamba Kanisa linashuhudia utendaji wa karama na kuziishi baraka za enzi ya Kimasihi hivi sasa, yaani leo. Hii ndiyo maana kuwa na mtazamo kamili na sahihi, yaani, mtazamo komavu kibiblia na kitheolojia juu ya Kanisa ni muhimu sana kwa ufahamu wowote wa kweli wa Ufalme. Angazia ukweli wa kibiblia ambao Petro aliutoa siku ya Pentekoste, kwamba Roho Mtakatifu katikati ya Kanisa ni utimilifu wa ahadi za Agano la Kale kuhusu enzi ya Kimasihi kuja miongoni mwa wanadamu, katika wakati wetu na katika siku zetu. Zingatia kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa majibu kulingana na malengo ya sehemu ya kwanza ya somo, hasa Kanisa kama mahala pa ufunuo, Roho, na uzima wa Mungu.
8 Ukurasa 78 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook Learn more on our blog