The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 3 3 5
UFALME WA MUNGU
Mtazamo wa Kanisa kama kituo unahusiana moja kwa moja na jukumu lake kama wakala wa Ufalme. Kama kituo ( locus ), Kanisa ni mahali ambapo karama na baraka za ufalme hupatikana kupitia Roho wa Mungu na uwepo wake; kama wakala, Kanisa ni chombo ambacho kwacho ujumbe na nguvu za ufalme wa Mungu hudhihirishwa na kutangazwa ulimwenguni. Kwa upande mmoja, Kanisa ni mpokeaji wa baraka za enzi ya Kimasihi, na kwa upande mwingine, ni chombo ambacho kwacho baraka za ufalme hupatikana katikati ya ulimwengu, ambamo sasa, kwa njia ya neema ya Mungu, fursa ya msamaha na upatanisho inatolewa. Kuzungumza juu ya Kanisa kama mahali au kituo pekee ni kulifanya Kanisa kuwa jumuiya iliyojitenga, na kufanya ionekane kana kwamba baraka za ufalme wa Mungu hutolewa kwa upendeleo. Kusisitiza uwakala wa Kanisa zaidi ya nafasi yake ni kuchanganya kazi ya Kanisa na ujio halisi wa Ufalme. Kanisa si Ufalme, wala haliwezi kwa uwezo wake lenyewe kuleta nguvu na utukufu wa Ufalme. Badala yake, kwa njia ya imani na utii kwa Yesu Kristo, Kanisa linakuwa njia ambayo Mungu anavamia enzi hii ya sasa kwa nguvu na upendo wa ufalme wake. Mtazamo wako hapa unapaswa kuwa wa kusisitiza kwamba Kanisa ni mahali (kituo) na wakala wa Ufalme. Kwa maneno mengine, maono ya Kanisa kama kituo ( locus ) yanapaswa kwenda sanjari na tafsiri ya Kanisa kama wakala wa Ufalme. Huu ni ufunguo wa ufahamu sahihi wa mwanafunzi juu ya jukumu na wajibu wa Kanisa ulimwenguni. Wajibu wa Kanisa kumwabudu Mungu ni kazi yake muhimu zaidi. Katika utambulisho wake kama ukuhani wa kifalme, wajibu wa Kanisa ni kutangaza fadhili zake Yeye aliyeliita kwa fahari na utukufu wake mwenyewe (rej. 1 Pet. 2:9-10). Kanisa lilizaliwa mara ya pili ili kusifu, kumpa Mungu wa Utatu thamani ambayo Yeye peke yake anastahili. Mpango wa ufalme, tangu mwanzo, ulikuwa ni kazi ya Mungu wa Utatu kama Shujaa wa Kimungu, akifanya agano na kufanya kazi ndani ya historia ya mwanadamu ili kurudisha enzi na utawala wake mwenyewe katika ulimwengu huu ulioanguka. Katika Yesu Kristo, Yehova amepigana vita na kushinda kwa mkono wake wa kuume ushindi mtukufu, na sasa, katika dunia nzima, ufalme wake unatoa fursa endelevu ya upatanisho. Kanisa la Yesu Kristo, kama wakala na msimamizi wake wa hadithi hii kuu, limezaliwa tangu mwanzo kwa sifa siku ya Pentekoste, ambapo wanafunzi walitangaza matendo makuu ya Mungu katika lugha zao (taz. Mdo. 2:13). Kwa ufafanuzi, Kanisa la Yesu Kristo ni jumuiya
9 Ukurasa 79 Muhtasari wa Sehemu ya 2
10 Ukurasa 80 Kipengele I
Made with FlippingBook Learn more on our blog