The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 3 6 /
UFALME WA MUNGU
ya ibada iliyoitwa na Mungu kuwa nyumba ya kiroho iliyonenwa na Mtume Petro, ule ukuhani mtakatifu ambao hutoa dhabihu za kiroho zinazokubalika kwa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo (1 Pet. 2:5). Tangu mwanzo kabisa, Kanisa limekusanyika mara kwa mara ili kumpa Mungu utukufu kwa ajili ya matendo yake makuu katika Kristo. Likichukua kwa hiari kielelezo cha ibada ya sinagogi, Kanisa la kwanza lilisoma na kufafanua Maandiko, lilitoa dua na maombi, kuimba zaburi, nyimbo, na nyimbo za rohoni, na kwa pamoja kushika maagizo (sakramenti) yaliyotolewa kwake na Kristo. Tangu mwanzo na daima siku zote, Kanisa limetoa kielelezo cha ushuhuda wa Ufalme katika ibada yake ya ushirika na sifa kwa Mwenyezi Mungu. Ni muhimu kwamba kila kizazi cha waamini kitumie uangalifu mwingi, juhudi nyingi, na nguvu nyingi katika kutafuta njia mpya na za kibunifu za kumtukuza Mungu, bila kuachana na njia za zamani. Utume wa Kanisa ni kipengele muhimu katika uwakala wake wa Ufalme wa Mungu. “Utume” (maana yake “iliyotokana na au ya mitume”) kama Kanuni ya Imani ya Nikea inavyosema, ni mojawapo ya alama kuu za Kanisa. Kama jumuiya ya mitume, Kanisa la Yesu Kristo, kama Waefeso 2:20 inavyosema, lenyewe linajengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na Yesu Kristo mwenyewe akiwa jiwe Kuu la Pembeni au Jiwe la Msingi. Mitume walikuwa wale ambao Kristo aliwachagua mwenyewe kuwa mashahidi walioshuhudia kwa macho ukuu na huduma yake. Jukumu la mashahidi hawa wa macho linatofautiana na jukumu la viongozi wengine wowote katika historia ya mwili, kwa sababu wao ni wa pekee katika uzoefu wao wa kipekee wa kuwa mashahidi wa macho wa kazi za Yesu ulimwenguni, na muhimu zaidi, ufufuo wake kutoka kwa wafu. (Tafadhali kumbuka vigezo vilivyowekwa na Mitume walipoamua kuchagua mtu wa kuchukua nafasi ya Yuda Iskariote kati ya wale kumi na wawili, taz. Matendo 1:11-). Mtu anaweza kuona jukumu la msingi ambalo Mitume wametekeleza katika maisha endelevu ya Kanisa kwa mfano wa kanoni, yaani vitabu vilivyochaguliwa kuwa sehemu ya Agano Jipya letu la sasa. Vizazi vya awali vya makanisa ya Kikristo viliamini na kusisitiza kwamba hati zetu za Agano Jipya ziliandikwa ama na Mitume au mtu fulani wa kuaminika aliyeambatana nao kwa karibu na kuidhinishwa nao. Tangu karne ya 19, wanazuoni wengi wabobevu wametilia shaka uandishi wa kitume wa sehemu kubwa ya Agano Jipya, ikijumuisha Injili nne, Matendo,
11 Ukurasa 81 Kipengele II
Made with FlippingBook Learn more on our blog