The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 3 7

UFALME WA MUNGU

Yakobo, 1 na 2 Petro, Yuda, na Ufunuo. Maswali mazito yanasalia miongoni mwa wasomi wa Biblia kuhusu uhakika wa kwamba Paulo ndiye aliyeandika vitabu vya Waefeso, Wakolosai, 1 na 2 Timotheo, Tito na Waebrania. Hata hivyo, licha ya yale ambayo wana-taaluma ya dini au wale wanaojiita wasomi wa Biblia wanaamini na kudai, na pia bila kujali hoja ya kwamba waandishi wa Injili na Nyaraka katika Agano Jipya ni akina nani hasa, Kanisa la Kristo liliviidhinisha vitabu vyetu vya sasa kuwa vya kitume, likivipa uzito na mamlaka ya Kitume, na kwa sababu hiyo, vinastahili kupewa heshima na imani yetu kikamilifu. Kile ambacho mfano huu unaonyesha ni kwamba Kanisa, bila kujali sayansi na/au usomi, kwa karne nyingi limeimarisha uaminifu na imani yake kwa kile lilichogundua kuwa kilitoka au kiliidhinishwa na Mitume. Kwa hiyo, Kanisa limetetea fundisho ambalo Mitume walipambania, na kihistoria limejihusisha tu na nyaraka hizo, elimu, mafundisho, na desturi ambazo zinaweza kuthibitishwa kuwa zilitokana na mafundisho na utendaji wa Mitume. Kuilinda imani yetu ni kuelewa kwamba ujumbe na utume wa Mitume ndio mamlaka ya mwisho kwa imani na utendaji wa Kanisa. Kama ilivyotajwa hapo awali, uthibitisho wa Kanisa kuwa mahali pa enzi ya Kimasihi na nguvu za Ufalme ni Roho Mtakatifu katikati ya Kanisa. Kama hekalu la Mungu Aliye Hai, waamini leo wanajengwa pamoja kuwa makao yanayofaa kwa Mungu wetu kukaa, kama makao ya Mungu katika Roho (Efe. 4:22). Kupitia nyara za Yesu juu ya maadui, amempa kila mwamini neema kulingana na mapenzi na kipimo cha Kristo mwenyewe (Efe. 4:7; rej. Rum. 12:3). Zaidi ya hayo, Paulo anasema kwamba Mungu ametoa watu wenye karama juu ya mwili wa Kristo; mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu (Efe. 4:11) ili kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi ya huduma ili mwili ukue, katika idadi na uhai wa kiroho. Ili kutekeleza kusudi hili, Roho Mtakatifu ametoa karama mbalimbali za uwezo wa kiroho kwa viungo mbalimbali vya mwili kwa ajili ya aina mbalimbali za wito na aina mbalimbali za huduma, kwa manufaa ya ushirika wa mwili (1Kor. 12:4-11). Madhihirisho haya ya neema, nguvu, na baraka yanahusishwa na utawala wa ufalme wa Mungu unaoonyeshwa sasa kupitia Agano Jipya (Yer. 31:31-; Eze. 36:14-; 26). Kupitia mwili uliovunjwa na kumwagika kwa damu ya Yesu, waamini sasa wanashiriki Roho wa Mungu (2 Kor. 3:6-), ambaye ni arabuni au “malipo ya

 12 Ukurasa 84 Kipengele IV

Made with FlippingBook Learn more on our blog