The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 3 8 /
UFALME WA MUNGU
awali” ya urithi wetu (2 Kor. 1:22; 5.5; Efe. 1:14), “malimbuko” na muhuri wa Mungu (2 Kor. 1:22; Efe. 1:13; 4:30). Kwa sababu ya ukweli huu wa hali ya juu na wenye kuzalisha shukrani ndani yetu, tunaweza sasa kutarajia Roho Mtakatifu kudhihirisha katikati ya Kanisa matendo ya nguvu, miujiza, baraka, mabadiliko, na uponyaji ambayo yanathibitisha ukweli kwamba enzi mpya tayari imepambazuka katika Yesu Kristo. Roho wa enzi ya Kimasihi amemiminwa, na maadui wa Mungu wanashindwa kupitia vita hai vya Kanisa la Mungu. Yesu atathibitisha Neno lake la kiungu katikati ya watu wake kwa ishara zinazofuatana nalo, ili watu wake mwenyewe wapate kuijua kweli ya Injili, na pia kupewa uthibitisho unaoonekana, usio na mashaka kwamba Yesu Kristo ndiye Bwana wa wote. Katika kuwaongoza wanafunzi katika sehemu iliyobaki ya somo hili, itakuwa muhimu kwako kutunza mkazo na uzingativu wako kuhusu lengo la somo katika maana ya jumla ya moduli ya Ufalme. Kwa kuzingatia mtazamo wa chini wa Kanisa wa wengi katika huduma, ni muhimu kwetu kujenga upya mtazamo bora zaidi wa kibiblia wa Kanisa. Kwa madhumuni ya somo letu la ufalme, tunaangalia majukumu pacha ya Kanisa kama mahali au kituo na kama wakala wa Ufalme wa Mungu ulimwenguni leo. Kama ilivyotajwa hapo awali, jukumu la Kanisa kama locus (kituo) limeungamanishwa kwa karibu na jukumu lake kama wakala. Katika mfululizo huu wa maswali, jitahidi kuwawezesha wanafunzi wako kugundua miunganiko mipya kati ya haya mawili. Usisite kuchunguza maswali yao juu ya vipengele maalum vinavyohusiana na somo, lakini ikiwezekana, sisitiza uhusiano huu wa kimsingi wa Kanisa katika jukumu lake kama maisha ya Ufalme na kama ushuhuda wa Ufalme. Kama kituo ( locus ), Kanisa linajionea maajabu ya Ufalme ambao linaushuhudia, na kama wakala Kanisa linaonyesha kikamilifu ukweli kwamba enzi ya Kimasihi imekuja katika Yesu, na lifanya hivyo kupiti ushuhuda wake, huruma, matendo ya miujiza na uponyaji, na ushuhuda na upendo wake. Angazia kweli hizi unapofanya marudio ya maudhui ya sehemu ya mwisho.
13 Ukurasa 86 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook Learn more on our blog