The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 3 9

UFALME WA MUNGU

Mifano hii Halisi imekusudiwa kuelekeza fikira za wanafunzi katika njia mahususi ambazo kwa hizo Kanisa linaweza kukutana na vikwazo katika azma yake ya kutimiza majukumu yake kama mahali na wakala wa Ufalme. Mojawapo ya maeneo haya muhimu yanayohusiana na hili ni swali la uadilifu: ni wakati gani, kwa hakika, tunapoonyesha kupitia matendo yetu, ibada zetu, na mahusiano yetu kwamba sisi ni mahali halisi pa Ufalme? Ni wakati gani ushahidi, matendo mema, na maajabu tunayofunua kwa majirani zetu yanatoa uthibitisho wa kweli kwamba sisi kama Kanisa tunajidhihirisha wenyewe kama wakala wa Ufalme? Moja ya mambo muhimu zaidi kuhusu hali ya kiroho ni uwezakano wake wa kuigizwa kwa namna bandia. Hata fimbo ya Musa iliigizwa na waganga na wachawi wa Misri. Jukumu letu kama wahudumu wa Injili na Kanisa ni kuomba kwamba Mungu atutumie kuwa mashahidi wa kweli wa habari za Ufalme katika maeneo yetu. Kwa maneno mengine, jukumu na shauku yetu lazima iwe kwamba Mungu atumie uhai na ushahidi wa makusanyiko yetu kuakisi jinsi utawala wake ulivyo duniani, kama huko mbinguni. Kwa kuwa Enzi ya Kimasihi imekuja katika Kristo, ni lazima tutoe ushuhuda wa uhalisia wa Ufalme, au kinyume chake tutabaki kuwa kiakisi duni cha jamii yetu. Kilicho muhimu kusisitiza na kuangazia katika mijadala yenu ni jinsi kutaniko linaweza kujua kuwa linatimiza wito wake kama kituo na wakala wa Ufalme. Mifano ifuatayo imekusudiwa kuangazia suala hili, na kutoa nafasi kwa uvumbuzi wenu wa pamoja. Kufikia mwisho wa somo la pili, unapaswa kuwa umewaeleza wanafunzi hitaji la wao kuwa wamefikiria na kufanya kazi ya msingi kwa ajili ya Kazi ya Huduma kwa Vitendo. Sasa, kufikia mwisho wa somo la tatu, unapaswa pia kuwa umesisitiza haja ya wao kuchagua kifungu kwa ajili ya Kazi yao ya Uchambuzi wa Maandiko (eksejesia). Kazi hizi zote mbili zina kawaida ya kuwashitukiza wanafunzi mwishoni mwa kozi, kwa hiyo hakikisha unawasisitiza kuhusu kazi zinazopaswa kufanywa, viwango vya kuzingatia wanapozifanya, na tarehe ambayo kazi zinatarajiwa kukamilika. Wape taarifa stahiki kuhusu kazi zao za mwisho na kazi nyingine zozote husika, na uwasihi wajipange na kuwa tayari kwa kazi hiyo kubwa iliyo mbele yao.

 14 Ukurasa 90 Mifano Halisi

 15 Ukurasa 92 Kazi

Made with FlippingBook Learn more on our blog