The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 3 4 1
UFALME WA MUNGU
Kukamilishwa kwa Utawala wa Mungu
MAELEZO YA MKUFUNZI 4
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa Somo la 4, Kukamilishwa kwa Utawala wa Mungu . Hili labda ni somo refu na gumu zaidi katika yote. Kiasi cha maudhui yanazoshughulikiwa katika somo hili ni kikubwa mno; hupaswi kudhani kuwa utaweza kukabiliana kwa urahisi na ugumu wote wa mambo yaliomo katika somo hili. Kusema kweli, Kanisa la Yesu Kristo, na wanazuoni na wanatheolojia wake wa kibiblia wacha Mungu zaidi, wanyofu zaidi na wenye uwezo zaidi wametofautiana juu ya maelezo mahususi ya mada juu ya masuala ya kifo, hali ya wafu, muundo wa ufufuo, unyakuo, na dhiki, achilia mbali mbingu. Wanafunzi wa darasa lako bila shaka hawatakuwa tofauti. Tarajia kiasi fulani cha kutokubaliana juu ya maelezo mbalimbali yanayohusiana na Ujio wa Pili na matukio yanayohusiana nao. Kiwango ambacho mtatofautiana bila shaka kitategemea misimamo ya kimadhehebu ya wanafunzi, mwelekeo wao wa kimafundisho, kiwango cha elimu ambacho wametangulia kuwa nacho kuhusu masuala haya, na uwezo wao wa kupima kwa umakini maoni yanayopingana na changamano za kitheolojia juu ya masuala yenye utata. Kilicho muhimu katika somo hili ni kweli muhimu zinazohusiana na nyakati za mwisho na mada za eskatolojia. Itakuwa muhimu kwako, kama aina ya mkufunzi na mwamuzi, kupatanisha maoni mbalimbali yanayotolewa na wanafunzi wako na maelezo ya msingi ya kitheolojia yaliyomo katika Kanuni ya Imani ya Nikea kuhusu Ujio wa Pili. Kwa maneno mengine, itakuwa muhimu kwako kusalia kwenye njia kuu ya kukamilishwa kwa Ufalme katika Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, na kupunguza kimakusudi aina mbalimbali zinazowezekana za tafsiri mbadala katika maelezo. Lazima kusudi lako la kitheolojia na kielimu lilenge kutoa «Picha Kubwa,” kwa kuwa ikiwa utaruhusu kuvutwa nje ya mada, hutaweza kudhibiti mwelekeo na muda wa kipindi chako kulingana na wingi wa mambo unayopaswa kuyaangazia katika somo hili. Hakuna muda wa kutosha kushughulikia maswali yote yatakayojitokeza, kwa hiyo itabidi utumie busara kadiri unavyoendelea. Lengo la moduli hii ya Ufalme wa Mungu ni kuwapa wanafunzi wako mtazamo wa kibiblia ili kuelewa kile ambacho Mungu anafanya katika historia ya mwanadamu, na kuwaandaa kuwa mashahidi wazuri wa Kristo na Ufalme wake. Somo hili la mwisho limejikita katika mawazo makubwa kadhaa ambayo ni muhimu katika kumalizia masomo yetu ya moduli ya Ufalme. Somo hili linahusu mada zote za kawaida zinazoangaziwa katika somo la eskatolojia katika juzuu za theolojia ya utaratibu, kwa maneno mengine, mafundisho ya mambo ya mwisho. Ndani yake
1 Ukurasa 97 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook Learn more on our blog