The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 4 2 /
UFALME WA MUNGU
utapata mafundisho kwa muhtasari kuhusu mawazo yote makuu yanayohusiana na mada hiyo ya eskatolojia – sababu zinazoonyesha umuhimu wa kujifunza eskatolojia, mada ya kifo, ufufuo, na hali ya wafu. Pia, somo linaangazia wahusika wa Ujio wa Pili, hukumu ya mwisho, na mbingu mpya na nchi mpya. Utakachotakiwa kufanya ni kuziangazia mada zote mahususi katika muktadha wa Hadithi ya Mungu. Sababu kubwa inayowafanya Wakristo wengi washindwe kufuatilia unabii kuhusu mambo yajayo ni kwamba wanasongwa sana na mambo mengi madogo madogo yaliyomo na kupoteza maono hayo mapana—Mungu Mwenyezi, kwa wakati na namna anayoijua Yeye, ameazimia kukamilisha mambo yote kupitia Kuja kwa Mwanawe duniani, ambaye ataondoa mabaki yote ya dhambi na kuanzisha mbingu mpya na nchi mpya ambamo Mungu anatawala milele. Hiyo ndiyo picha kuu kuliko zote, na ndiyo unayopaswa kutafuta kuangazia wakati wote wa kujifunza somo hili. Tafadhali, angalia tena katika malengo kwamba kweli hizi zimeelezwa kwa uwazi. Kama kawaida, jukumu lako kama Mkufunzi na mshauri ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na muda wa kukaa kwako pamoja na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo uwezekano wa wanafunzi kufahamu ukubwa wa malengo haya unavyozidi kuwa mkubwa. Ibada hii inashughulika na jambo lililotolewa mwanzoni mwa maelekezo haya kwa mkufunzi, yaani, kwamba lengo la somo la eskatolojia linapaswa kuwa juu ya njia tunazomwona Mungu akikamilisha mpango wake kupitia Mwanawe, badala ya kujikita katika uchambuzi wa mambo madogo madogo ambamo akili ya mwanadamu, kupitia uvivu na udadisi wake, ina mwelekeo wa kutangatanga. Kwa maneno mengine, andiko hili linafunua ukweli kwamba kiini cha kile ambacho Mungu anataka kufanya katika kufikisha Hadithi yake kwenye hitimisho lake ni kuzingatia adhama na fahari ya Mwanawe, ambaye peke yake ndiye ambaye Baba alimwona kuwa anastahili kuleta mwisho wa mambo yote. Hili si wazo la ibada tu; badala yake, ni theolojia ya ndani kabisa tunayoweza kujifunza. Katika Yesu wa Nazareti sasa tumepewa kumwelewa yule ambaye kupitia kwake Mungu atawahukumu walimwengu na kurudisha mambo yote kwenye ubora na utukufu wa kabla ya Anguko. Amepewa mengi, lakini, kama Bwana wa yote, anaweza na atatimiza mengi. Hapa ndipo tunapofikia kuelewa jukumu la Yesu kama Mpakwa
2 Ukurasa 97 Ibada
Made with FlippingBook Learn more on our blog