The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 3 4 3
UFALME WA MUNGU
Mafuta wa Baba, yule aliyechaguliwa na Mungu ili kurejesha ulimwengu huu chini ya utawala wake, na yule ambaye kwa kweli atatawala milele kwa amri ya Mungu. Kama isemwavyo, “Jambo kuu ni kuweka jambo kuu kuwa jambo kuu.” Hii ni kweli zaidi linapokuja suala la kujifunza masuala na mada zinazohusiana na nyakati za mwisho. Tafadhali, angalia tena katika malengo kwamba kweli hizi zimeelezwa kwa uwazi. Kama kawaida, jukumu lako kama Mkufunzi na mshauri ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na muda wa kukaa kwako pamoja na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo uwezekano wa wanafunzi kufahamu ukubwa wa malengo haya unavyozidi kuwa mkubwa. Ingawa sehemu kubwa ya ufunuo wa Mungu katika Biblia inahusishwa na kugundua mapenzi ya Mungu kwa uumbaji wake katika utimilifu ujao wa mambo yote, mtazamo wa haraka katika mafundisho na mahubiri ya Kanisa la kisasa unaonyesha kupuuzwa kwa uhalali wa unabii. Mahubiri yetu, mitaala ya kujifunza Biblia, ushauri, mafundisho, na huduma za kuabudu ni mara chache sana maudhui yake yanahusisha madokezo yoyote juu ya Kuja kwa Yesu Mara ya Pili. Katika makanisa mengi, wachungaji wamekwenda kwa miezi hata miaka bila kurejelea kukamilishwa kwa Ufalme. Moja ya malengo muhimu ya muda wako pamoja katika kipindi hiki ni uwezo wako wa kuwafanya wanafunzi wako kuelewa kiwango cha umuhimu ambacho mafundisho haya yanao kwa habari ya maadili yetu, theolojia yetu, na huduma yetu. Mifano iliyopo hapa chini inaanganiza tatizo la Kanisa kutozingatia mada nyeti na muhimu ya Ujio wa Pili wa Kristo. Mifano hii pia inaangazia baadhi ya njia ambazo kwa kawaida tunaelekea kufikiria kuhusu masuala makuu yanayohusiana na kurudi kwa Kristo. Ndani ya makanisa kuna aina tofauti tofauti za miitikio, ikiwa kwa upande mmoja ni pamoja na kutojali kabisa unabii wa kibiblia na kwa upande mwingine ni aina fulani ya kuzingatia kwa kupitiliza mambo yanayohusiana na nyakati za mwisho. Lengo ni kuwasaidia wanafunzi wako, ambao wengi wao wanahudumia wengine katika maeneo ya mijini, kuelewa kwa nini Mungu alitupa moduli hii, na ni tofauti gani ya kivitendo nyenzo hii inaweza kuleta maishani mwetu na katika huduma zetu tunapoitendea kazi ipasavyo.
3 Ukurasa 99 Kujenga Daraja
Made with FlippingBook Learn more on our blog