The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 4 4 /

UFALME WA MUNGU

Ni muhimu kutambua kwamba katika maana moja kukamilishwa kwa Ufalme kunahusiana moja kwa moja na daraka la Yesu mwenyewe kama Mfalme. Kwa maneno mengine, Baba ametoa mamlaka yote mbinguni na duniani kwa Kristo (rej. Mt. 28:18), na hivyo, Kristo akiwa Bwana Mshindi ana mamlaka na amri ya kukomesha masalia yote ya uasi, dhambi, na uovu, kama Bwana mteule na Mpakwa Mafuta wa Baba. Ni Mungu ambaye amemtukuza Kristo sana, na kumpa jina lipitalo majina yote katika ulimwengu huu na ujao, ambaye mwenyewe atahakikisha kwamba kila goti linapigwa na kila ulimi ukiri kwamba Yesu ni Bwana, kwa utukufu mkuu wa Baba (Flp. 2:9-11). Akiwa Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme, Yesu sasa anachukua cheo chake kama mtekelezaji wa mapenzi ya Baba, na kuwaita kutoka katika ulimwengu watu kwa ajili yake mwenyewe, ambao ni wake peke yake na walio na bidii kwa ajili ya matendo mema (Isa. 55:5; Yoh. 10:16, 27; Tito 2:11-15). Akiwa Mkuu wa Kanisa anayetawala, anatembea kati yao, akiwapa karama na viongozi anaowachagua mwenyewe, akiwatawala kupitia shauri lake la moja kwa moja na uweza wake kwa njia ya Roho Mtakatifu (1Kor. 5:4-5; 12.28; Efe. 4:11-12; Mt. 28:19-20; 18:17-18; 301; 2 Tim. 5:20; Tito 3:10). Akiwa Mchungaji-mlinzi, analilinda na kutegemeza kundi lake katika kila hali wanayokabiliana nayo, akiwasaidia kushinda katikati ya majaribu na mateso yao yote (Ebr. 13:20-22; 2 Kor. 12:9-10; Rum. 8:35-39). Kama Shujaa wa Kiungu aliyepaa hadi kwenye cheo cha utukufu na heshima kwenye Mkono wa kuume wa Baba, Bwana wetu anazuia na kuwashinda maadui wote wa Mungu, na kufanya halisi katikati ya Kanisa baraka za enzi ya Kimasihi ambayo yeye binafsi aliianzisha (Mdo. 12:17; 18:9-10; 1 Kor.15:25). Akiwa Mungu Mwenye Nguvu na Mwana Mshindi kwa amri ya Baba, anasimamia utume wa Kanisa lake, ambalo ameliamuru kwenda hadi miisho ya dunia kushuhudia amani na upatanisho ambao ameupata kwa ajili ya wanadamu wote kupitia kifo chake Msalabani (Mdo. 28:19 20). Hatimaye, hukumu yote imewekwa mikononi mwake (Yoh. 5:22-23); Yeye ndiye aliyeteuliwa kuwaangamiza adui za Bwana na kuwapa thawabu watakatifu wa Bwana, na ndiye aliyechaguliwa na Mungu kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kulipiza kisasi juu ya wale wasiomjua Mungu na wasioitii Injili (Zab. 2:9; Isa. 9:6-7; Ufu. 19:11-21; 2 Thes. 1:8). Nukuu hizi zote zinaelekeza kwenye ukweli mmoja mkuu: kukamilishwa kwa Ufalme ni udhihirisho wa nafsi ya Yesu kama Mwana wa Adamu, yule ambaye ameteuliwa na Mungu kurudisha ulimwengu hatimaye chini ya utawala wa Mungu,

 4 Ukurasa 100 Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook Learn more on our blog