The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 4 5

UFALME WA MUNGU

kusahihisha makosa yote, na kukomesha maumivu yote. Yesu ndiye ambaye amepewa utume wa kuwakilisha masilahi ya Baba bila kikomo au mipaka. Hii ndiyo “picha kubwa” ya utimilifu, na sababu ya kwa nini mazungumzo yoyote makini kuhusu kukamilishwa kwa Ufalme lazima yamlenge Yesu, na yasijielekeze katika maana ya vichwa saba na pembe kumi juu ya joka katika Ufunuo 12. Hii haimaanishi kwamba hatupaswi kutafuta maana ya unabii maalum tuliopewa kupitia uvuvio wa Roho Mtakatifu; badala yake, ni kusema kama malaika alivyomwambia Mtume Yohana katika Ufunuo ule kwamba kiini cha unabii ni ushuhuda wa Yesu (Ufu. 19:10). Mada ya eskatolojia kwa kawaida hupatikana katika juzuu ya mwisho ya theolojia ya utaratibu, na kwa kawaida imeainishwa kama somo la “mambo ya mwisho” (Kiyunani eschata ). Wanatheolojia na wanazuoni kwa kawaida hugawanya maelezo yao kuhusu mambo ya mwisho katika makundi mawili mapana, yakishughulika na masuala ambayo yanahusiana ama na watu (ambayo huelekea kuzingatia masuala ya kifo, ufufuo, hukumu, na maisha ya baada ya kifo) au masuala yahusuyo ulimwengu (yaani, hali ya jamii nzima ya binadamu, viumbe vyote hai na visivyo hai, na hatimaye uumbaji katika ujumla wake). Wakati mwingine unaona katika kazi za kitheolojia kwamba eskatolojia ya ulimwengu inafungamana na matukio na masuala yanayohusiana na mwisho wa dunia. Elimu ya aina hii, hata hivyo, si nzuri au ya kuaminika kama zile tafsiri zinazoeleza mtazamo wa ulimwengu mzima, kwa sababu maneno yanayotumika katika matumizi ya Biblia, kama vile neno la Kiebrania be’aharit hayyamim (ambayo katika Septuagint [LXX] limeandikwa “ en tais eschatais hemerais,” “katika siku za mwisho”), yanaweza kuwa na maana ya “mwisho wa enzi au ulimwengu wa sasa,” au hata “baada ya hapo” katika lugha ya jumla. Mtazamo wa kibiblia kuhusu wakati kwa kweli unaathiri uelewa wetu wa eskatolojia. Bila shaka, wazo la kibiblia la wakati haliutazami wakati kama mzunguko (ikimaanisha kwamba eskatolojia ingezungumza tu kuhusu matukio katika kukamilika kwa mzunguko fulani), wala halitazami kama tunavyoelekea kufikiria kuhusu wakati, katika mtazamo wa “mstari” au mtiririko wa matukio (kwa maana kwamba eskatolojia haitaweza kutazama mambo katika muono endelevu). Ingekuwa bora zaidi kusema kwamba maoni ya Biblia kuhusu wakati ni aina ya utaratibu unaorudiwa ambapo ghadhabu ya Mungu na neema yake huingiliana pamoja hadi utaratibu wa kusudi na mapenzi yake mwenyewe unapojulikana. Hivyo

 5 Ukurasa 100 Kipengele I

Made with FlippingBook Learn more on our blog