The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 4 6 /
UFALME WA MUNGU
basi, eskatolojia inapaswa kutazamwa katika muono wa uendelevu au mtiririko wa matukio. Inaweza kuzungumza juu ya utimilifu wa Ufalme kwa njia tofauti tofauti, iwe ni kwa habari ya mwisho wa ulimwengu, mwisho wa mhusika, au chochote. Kilicho muhimu ni kwamba tunapojadili masuala yanayohusiana na mwisho wa dunia, tunapaswa kujua kwamba kwa faida ya majadiliano, tunazielekeza katika kipengele fulani mahususi kwa ajili ya kujifunza. Katika uhalisia, hata hivyo, wakati Ufalme utakapokamilishwa, matukio na hali nyingi zinazoelezewa kupitia mada hizi mbalimbali zitakuwa zikitokea kwa wakati mmoja, na hii inafanya kuwa vigumu sana kubainisha nyakati maalum kwenye mstari (kama ilivyokuwa) kuhusu mwelekeo wa mwisho wa nyakati. Kwa hiyo, ushauri bora zaidi katika kushughulika na masuala ya nyakati za mwisho, ni kukumbuka hekima nzuri ya Kumbukumbu la Torati 29:29: mambo ya siri (ya wakati maalum, mahali, tukio la nyakati za mwisho) ni ya Bwana, lakini mambo yaliyofunuliwa (yale makubwa, masuala makubwa, kwa mfano, uhakika wa kurudi kwa Yesu) ni yetu. Unabii huu si kwa ajili ya kujibu maswali ya udadisi wetu, bali ni ili kwamba tuweze kuishi kwa kufahamu kweli zinaowasilishwa. Utimilifu wa Ufalme, kwa njia nyingi, ni kumshinda huyu, adui wa mwisho, ambaye ni mauti (1Kor. 15:54-56). Katika Agano la Kale, kifo mara nyingi kilichukuliwa kama sehemu ya asili ya maisha ya mwanadamu. Kifo kiliingia ulimwenguni kupitia kutotii kwa Adamu na Hawa, na bado, maisha ya mwanadamu kupitia Adamu hayakutazamwa kuwa ya kutoweza kufa, lakini kama yenye uwezekano fulani wa kudumu, kwa msingi wa uwezo wa wanadamu kutii utawala wa Mungu. Mara nyingi, lengo lililozungumzwa katika mtazamo wa maisha ya Agano la Kale ni mtu kuishi maisha marefu, kamili pamoja na wapendwa wake, na kufa kwa heshima na amani, sio kwa sababu ya aibu na ufisadi. Kufa mapema kwa kawaida kulionwa kuwa ni uovu mkuu (2 Wafalme 20:1-11), na ni tendo lililochukuliwa kuonyesha aina fulani ya hukumu kutoka kwa Mungu kutokana na uovu au dhambi (Mwa. 2-3; Kum. 30:15; Yer. 21:8; Eze. 18:21-32). Kifo, hata hivyo, kilibeba hisia ya kutisha, kwani kufa ni kutengwa na wapendwa wako, kutengwa na ibada, na watu wa Mungu, na kutengwa na Mungu mwenyewe (Zab. 73:23-28; 139.8). Kwa sababu ya haya na mengine mabaya yanayohusiana na kifo, kujiua kulikuwa nadra miongoni mwa watu wa Mungu (1 Sam. 31; 2 Sam. 17:23), na adhabu ya kifo (yaani hukumu ya kifo) ilichukuliwa kuwa kali na ya kutisha.
6 Ukurasa 102 Kipengele II
Made with FlippingBook Learn more on our blog