The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 4 7

UFALME WA MUNGU

Katika Agano Jipya, na mkazo wake wa wazi wazi juu ya Ufalme wa Mungu katika Yesu Kristo, wazo la kifo linachukuliwa kuwa tatizo la kitheolojia. Uhai hutoka kwa Mungu, ambaye peke yake ana uzima katika nafsi yake mwenyewe, chemchemi za kutopatikana na mauti (1 Tim. 6:16). Wanadamu wako chini ya kifo, si tu kwa sababu ya hali yao ya asili kama viumbe wenye makosa, walioumbwa, bali kwa msingi wa hali yao ya dhambi pamoja na kuwa chini ya laana wanayoshiriki na wengine wote kwa sababu ya uhusiano wao na Adamu (taz. Rum. 6:23; 5:12-). Kwa sababu ya uhusiano huu na hukumu, wanadamu wanaishi katika hofu ya kifo kinachotokana na laana (Mt. 4:16; Ebr. 2:15). Kwa hiyo, kwa kuwa Bwana Mungu peke yake ndiye mwanzo na chemchemi ya uzima wote (Rum. 4:17), tunakufa kwa sababu kwa namna fulani tumetengwa na uzima wa Mungu; kutengwa kulikotokea kutokana na uasi wa Adamu dhidi ya utawala wa Mungu, na sasa kupitia kwake kutengwa huko kumetupata sote (Rum. 5:15, 17-18; 1 Kor. 15:22). Sisi sote, kama wanadamu walioanguka na kutengwa, tunashiriki katika dhambi zetu wenyewe na hukumu inayofuata juu yetu (Rum. 3:23; 5:12), na tumejiletea hukumu na matokeo ambayo kifo kinawakilisha (Rum. 6:23; Ebr. 9:27). Hivyo basi, ukweli kuhusu kifo katika eskatolojia ya mtu binafsi na ya ulimwengu, ni nguvu, kani inayotokana na uasi wa uzao wa wanadamu ulimwenguni, ambao unagusa maisha ya watu wote. Kifo si tu matokeo ya asili ya uzee na uchovu; bali ni matokeo ya kutengwa na Mungu kutokana na sisi wenyewe kukataa mamlaka na utawala wake maishani mwetu. Ni kutengwa na Mungu. Katika hali fulani ya kusikitisha, maisha yote ya mwanadamu hadi kiini chake yamehusishwa katika athari ya dhambi ya Adamu katika mwili (Rum. 8:6; 1 Yoh. 3:14), na mwelekeo huo wa dhambi unabaki ndani yetu licha ya nia yetu ya kushika sheria ya Mungu (Rum. 7:9; 1 Kor. 15:56; Yak. 1:15). Kama baba wa uongo na uasi, shetani anaonekana katika Agano Jipya kama bwana wa mauti (Ebr. 2:14), na katika maeneo fulani, kifo chenyewe kinaweza kuonekana kama nguvu ya kishetani (1 Kor. 15:26-27; Ufu. 6:8; 20:13-14). Kifo kitafanywa kuwa batili wakati wa Ujio wa Pili wa Kristo, ambaye kifo chake msalabani kimevunja nguvu za mauti, na kuwapa wale wanaomtumaini taraja la kuishi milele kwa njia ya imani katika yeye (Yoh. 11:22-23; 1Kor. 15:54-58).

Made with FlippingBook Learn more on our blog