The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 4 8 /

UFALME WA MUNGU

Katika mazungumzo yako yote na wanafunzi juu ya nadharia mbalimbali zinazohusu hali ya kifo, ni muhimu kuangazia kipengele kikuu cha tumaini kinachohusishwa na ushindi wa ufalme wa Yesu Kristo. Kwa maneno mengine, kazi ya Yesu msalabani haikuwa kutupa mada za ziada za theolojia ili tujadili, bali kutupa ukweli dhahiri, wazi, na usiopingika ambao juu yake tunaweza kujenga na kutegemeza maisha yetu, na ambao unaweza kutoa tumaini kwa ajili yetu na kwa ajili ya wengine katikati ya ulimwengu ambamo maelfu ya watu hufa kila siku, mara nyingi wakiwa na tumaini dogo au bila tumaini kabisa na bila ufahamu wa kile ambacho Baba mwenye upendo Mungu amewafanyia kupitia Mwanawe. Habari njema za Ufalme wa Mungu katika Kristo ni kwamba yeye mwenyewe, ambaye hakuhitaji kufa wala hakuwa chini ya wajibu wowote wa kusaidia nafsi zetu zenye dhambi kufikia uhusiano mpya na Mungu, alishiriki kikamilifu katika kifo cha kibinadamu kwa ajili yetu (Flp. 2:7; 1 Kor. 5:7; 1 Pet. 3:18). Mwanzilishi wa uhai na uumbaji akawa mwanadamu na kufa; alikufa “kwa ajili yetu” (Mk. 10:45; Rum. 5:6; 1 Thes. 5:10; Ebr. 2:9). Kulingana na neno la Mitume, Bwana kupitia kifo chake alimponda shetani na kukishinda kifo chenyewe, na sasa anazo funguo za kuzimu na mauti (Ebr. 2:14-15; Ufu. 1:17-18). Yeye peke yake alivunja mtego wa kifo kwa wale wote ambao kwa imani wameunganishwa naye kwa “kubatizwa katika Kristo” (Rum. 6:3-4). Kupitia umoja huu tulionao pamoja na Bwana mfufuka, tumekufa pamoja naye kwa habari ya dhambi na kwa habari ya ulimwengu (Rum. 7:6; Gal. 6:14; Kol. 2:20). Katika Yesu Kristo kila mwamini amepitia njia ndefu ya kifo; ndani yake tulionja ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi zetu, na ndani yake tumepata adhabu yake halisi, aibu, na msiba kamili (2 Kor. 4:10; 5:14-15; Kol. 3:3). Kwa maneno mengine, matokeo ya huduma ya Yesu yalikuwa ni kuunganisha hadhi, historia, na maisha ya kila mwanadamu na maisha yake mwenyewe, na sasa, wale wanaomtumaini kwa imani, wanawekwa huru “katika Kristo.” Sisi tulio wa Yesu kwa imani tumepita kutoka mautini kuingia uzimani ndani yake (Yohana 5:24). Kwa sababu ya umoja wetu naye, hatutawahi kuonja kifo halisi (Yohana 8:51-52). Hii ni tofauti sana na ulimwengu, ambao hauna Mungu na Kristo na kwa sababu hiyo tayari umekufa (Ufu. 3:2), na tayari umewekewa mwisho wa kutisha wa kutengwa mbali na Baba, hali ambayo Yohana anaitaja kama kifo kikubwa, kifo cha pili (Ufu. 20:14). Kama wanadamu, wanafunzi wa Yesu bado tuko chini ya madhara yale yale ya laana kwenye miili yetu (yaani tunakufa, tunaugua magonjwa, sisi ni wahasiriwa wa vurugu, tunakuwa walemavu, nk). Kwa kweli tutakufa ikiwa hatutaishi hata siku ya

 7 Ukurasa 106 Kipengele III

Made with FlippingBook Learn more on our blog