The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 3 4 9
UFALME WA MUNGU
mwisho ambapo walio hai watakaosalia watabadilishwa kama inavyozungumzwa katika 1 Wakorintho 15. Hata hivyo, wale waamini wanaokufa kimwili, wanakufa “katika Kristo” (1 Thes. 4:16) au “wanalala usingizi” (Mdo. 4:13-15). Hiki si kifo katika maana ya kusikitisha sawa na wale ambao wametengwa na uzima wa Mungu. Kifo cha kimwili kipo kwa Mkristo, lakini ukatili wake umetoweka maana hakuna tena chochote kinachoweza kumtenganisha Mkristo na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana (Rum. 8:35-39). Ni ajabu iliyoje kwamba, sasa, kifo kinaondoa utaji (kiambaza) kati ya Mkristo na Bwana wake, na kuuacha uhai huu ni kusafirishwa hadi kwenye uwepo wa Yeye ambaye alionja kifo kwa ajili ya kila mtu (2 Kor. 5:1-10; Flp. 1:20-21), na ambaye atawafufua tena waamini wote waliokufa ili wafurahie amani isiyo na mwisho katika mbingu mpya na nchi mpya. Hii ndiyo maana ya utimilifu wa Ufalme kwa sisi tunaoamini (1 Kor. 15:20; Kol. 1:12). Maswali haya yameundwa ili kuangazia mambo makuu yanayohusiana na sehemu ya kwanza ya video. Kumbuka ushauri mzuri uliotolewa hapo awali, na ukazie fikira njia ambazo maswali mbalimbali yanaweza kutusaidia kuelewa ukuu wa Kristo katika ukamilisho wa Ufalme. Kwa maana moja, masuala yote ya utimilifu wa Ufalme hatimaye ni masuala ambayo yanahusiana na Yesu Kristo. Zingatia maswali ambayo wanafunzi wako wanayo kuhusu somo hili, lakini hakikisha kwamba wanaelewa kuwa mtazamo wa Kristo wa nyakati za mwisho ni ufunguo mkuu wa kuelewa utimilifu wote wa ufunuo wa Mungu kuhusiana na mada hizi. Kanisa la Yesu Kristo limeunganishwa kihalisi na Kristo, ambaye nafsi yake, kazi zake, na faida zake vinatupata sasa kwa imani, kwa njia ya Roho Mtakatifu. Ukweli huu uwe kiini cha uwasilishaji wako na mjadala wa maelezo ya eskatolojia sasa.
8 Ukurasa 111 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Ni muhimu kutambua maneno mbalimbali ambayo wanatheolojia hutumia wanapozungumza juu ya ujio na/au madhihirisho ya Kristo ulimwenguni.
9 Ukurasa 112 Kipengele I-A
Parousia (Siku ya Bwana)
Huenda hili ndilo neno linalotumiwa mara nyingi zaidi kuhusu Ujio wa Pili wa Yesu, na kihalisi humaanisha “kuwa pamoja na.” Linamaanisha “kuwapo, kuja, au kuwasili.” Paulo anatumia neno hili katika 1 Wathesalonike 4:15 kuashiria kuja kwa Yesu kuwafufua wafu wenye haki na kuwanyakua (yaani unyakuo) ili
Made with FlippingBook Learn more on our blog