The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 5 0 /

UFALME WA MUNGU

kuwa pamoja naye milele. Neno hilo pia linahusishwa na awamu ile ya kuja kwake ambayo inahusisha kuangamizwa kwa mtu wa kuasi, mpinga-Kristo (2 Thes. 2:8). Parousia sio siri au tukio la uficho, bali ni ufunuo na udhihirisho wenye utukufu. Neno hili pia linahusishwa na maana yake ya kimaadili; kulingana na maagizo ya Paulo, waamini wanapaswa kujiweka tayari, kumwomba Mungu ili wapate neema yake itiayo nguvu ili wasiwe na lawama katika utakaso mbele za Mungu Baba siku ya parousia ya Bwana Yesu pamoja na watakatifu wake wote (1 Thes. 3:13). Neno hili la Kiyunani linamaanisha “ufunuo.” Mtume Paulo anatoa changamoto kwa kanisa la Korintho linapongojea “kufunuliwa ( apokálypsi ) kwa Bwana wetu Yesu Kristo” (1Kor. 1:7). Neno hilo linaonekana pia katika 2 Wathesalonike 1:6-7 na 1 Petro 4:13, na maandiko yote mawili yanaonyesha kwamba apokálypsi itakuwa wakati wa hukumu kuu ya Mungu juu ya maadui wa Mungu, na shangwe kuu kwa wale wanaongojea kufunuliwa kwake. Kwa maana moja, maana hii inabadilisha kila kitu tunachojua kuhusu Ujio wa Pili. Neno hili hubeba maana ya “madhihirisho.” Yesu atakapofunuliwa au kudhihirishwa mwishoni mwa kipindi cha dhiki kuu, atadhihirisha utukufu wake ulimwenguni, na matokeo yake ni hukumu ya maadui wa Mungu, na thawabu kwa wale ambao wameweka tumaini lao kamili katika kufunuliwa kwake, na wamengojea kwa saburi thawabu zinazohusiana na kutokea huko (1 Tim. 6:14; 2 Tim. 4:8). Ni kukamilika kwa wokovu wao (Tito 2:13-14). Orodha ya sifa zinazotajwa hapa inawakilisha kiini cha madai muhimu, ya kiinjili, na ya kihistoria yaliyotolewa kuhusiana na Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Kwa mara nyingine tena, ingawa kuna madai mengi madogo kuhusu kuja kwake ambayo yamekuwa na yataendelea kubishaniwa katika miktadha mbalimbali ya kitheolojia na kitaaluma, kiini cha mafundisho kuhusu kuja kwa Yesu yanashughulika na nafsi yake, yaani Kristo mwenyewe, na matendo yake mwenyewe yanayohusika na ujio huo. Hili ni muhimu kwa ajili ya kuwawekea msingi waamini wapya katika kiwango cha chini cha msingi kinachoonekana kuwa muhimu kwa imani kulingana na Kanuni ya Imani. Zaidi ya hayo, hata pale ambapo wale wanaopokea mafundisho Apokálypsi Epipháneia (Epifania)

 10 Ukurasa 113 Kipengele I-C

Made with FlippingBook Learn more on our blog