The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 5 6 /

UFALME WA MUNGU

namna yoyote ambayo ukweli kuhusu kukamilishwa kwa Ufalme unaweza kuathiri maisha yao kwa njia chanya. Ni lazima tujitahidi kuwasaidia Wakristo watenda-kazi, wachungaji, na wahudumu wa mijini kurejesha tumaini la Ufalme kupitia maandiko na mafundisho haya ya kibiblia. Kwa hiyo, tunapochunguza matokeo ya mafundisho haya, jaribu kuzingatia njia ambazo mafundisho haya yanaweza kurejeshwa kwa uhakika katika mazingira ambayo, kwa sehemu kubwa, yameweka kando mafundisho ya kiapokaliptiki ya Kanisa. Bila shaka, sehemu hii ya somo inapaswa kuongozwa na maswali na hoja za wanafunzi. Hata hivyo, hitaji hili la kuyawezesha makusanyiko kuamka kuhusiana na theolojia ya tumaini la utimilifu wa Ufalme ni muhimu sana. Sasa, kazi yako kama mwalimu na msahihishaji itapaswa kuanza kwa bidii. Tafadhali hakikisha kuwa umepokea mapendekezo ya wanafunzi wote kuhusu kazi zao za huduma, kazi za Ufafanuzi wa Maandiko na taarifa nyingine kwa pamoja kwani hili litakuwezesha kubainisha jumla ya maksi za mwanafunzi. Tena, busara yako kuhusu kazi zitakazochelewa inaweza kuamua kwa urahisi ikiwa unakata alama za wanafunzi, na kusababisha mabadiliko ya daraja la ufaulu, au kuwapa wanafunzi alama ya “Haijakamilika” hadi kazi ikamilike. Vyovyote utakavyotekeleza kanuni zako kuhusiana na kazi zao, kumbuka kwamba kozi zetu kimsingi hazihusu maksi ambazo wanafunzi wanapata, bali ile lishe ya kiroho na mafunzo ambayo kozi hizi zinatoa. Pia, hata hivyo, kumbuka kwamba kuwasaidia wanafunzi wetu kujitahidi kupata matokeo bora ni sehemu muhimu ya masomo yetu. Hongera, mmekamisha moduli ya Capstone ihusuyo Ufalme wa Mungu. Tunasherehekea pamoja nanyi, kama watenda kazi pamoja katika Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Umewaongoza wanafunzi wako kupitia dhana fulani ngumu, na kuwatia moyo kupitia yale ambayo bila shaka ni mojawapo ya mafundisho muhimu zaidi katika Neno la Mungu kwa ujumla wake—Ufalme wa Mungu na Kristo. Ombi letu la dhati ni kwamba uwekezaji ulioufanya katika mioyo na akili za wanafunzi wako usirudi bure kwa Bwana, bali uzae matunda tele na ya kudumu kwa ajili ya Yesu Kristo kupitia juhudi zako, maombi, na kazi yako. Mungu akubariki sana unapoendelea kuandaa viongozi wa kanisa la mjini!

 17 Ukurasa 134 Kazi

 18 Ukurasa 135 Neno la Mwisho kuhusu Moduli hii

Made with FlippingBook Learn more on our blog