The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 5 5

UFALME WA MUNGU

Mt. 5:29, 30; 10:28; Rum. 35; 51; 5:11). Hatutaishi bila miili katika Ufalme mpya wa Kristo, lakini hatutahitaji lishe ya kimwili ili kututegemeza (Rum. 14:17), wala kuendeshwa na tamaa ya kujamiiana au ngono (Mt. 22:30; Mk. 12:25; Lk. 20:35). Taswira ya Ufalme katika Agano Jipya imejaa mifano mingi kuhusu wazo la karamu, na Yesu aliahidi atakunywa pamoja na wanafunzi wake tunda la mzabibu katika Ufalme (Mt. 26:29). Picha za uwepo wetu katika uumbaji mpya wa Mungu ni za kupendeza sana: tutafurahi milele katika uwepo wa Mungu kama watumishi wake, wanaoishi katika mji wake, wakitawala mataifa sawa sawa na mapenzi yake (Luka 19:17; Mt. 25:20-21). Hapo tutamtumikia katika mji uliobuniwa kwa mawazo yake mwenyewe, na tutaelewa jinsi tunavyoeleweka (1Kor. 13:12). Tutafananishwa na sura ya Yesu, katika utukufu na fahari yake yote, na tutamwona jinsi alivyo (1 Yohana 3:2). Kwa namna fulani ya ajabu, tutabadilishwa ili tuhusiane kwa karibu na Bwana wa Majeshi, kama Bwana wetu anavyohusiana naye (Isa. 6:3; Ufu. 4:8). Naam, tutakaa katika makao yake milele (Yohana 14:2), mji wa Mungu Aliye Hai, Yerusalemu wa mbinguni (Ebr. 12:22), tukiuona upendo wake na kusudi lake, tukiwa watu wake, na yeye akiwa Mungu wetu (Ufu. 21:3). Kwa mara nyingine tena, zingatia njia ambazo kazi ya Yesu inaonekana katika utimilifu wa Ufalme wa Mungu. Ingawa uzingatiaji mzuri na wa wazi wa maswali mbalimbali ya wanafunzi unafaa, unahitaji kujikita zaidi katika mkazo wa somo hili ambao ni Kristo. Kipekee, zingatia mkazo wa maswali ya msingi yaliyomo tayari katika kozi hii. Kwa maneno mengine, tafuta kuunganisha majibu yaliyotolewa katika kozi nzima, na uone jinsi Mungu, katika utimilifu wa Ufalme, anatatua masuala, matatizo, na mahangaiko mbalimbali ambayo Anguko lilisababisa. Mifano hii Halisi inatafuta kusisitiza umuhimu wa kweli hizi katika maisha ya Kanisa kupitia mifano iliyotolewa. Inaonekana kuna aina fulani ya mtazamo finyu wa unabii katika makusanyiko mengi ya kiinjili. Wakiwa wamezimwa kwa kiasi kikubwa na mikutano na mikazo mingine ya kimafundisho juu ya unabii ambayo hutafuta kupatanisha matukio mbalimbali ya sasa na unabii wa Biblia, wengi wanaonekana kukatishwa tamaa kwa habari ya kuamini tena endapo kuna

 15 Ukurasa 128 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

 16 Ukurasa 132 Mifano Halisi

Made with FlippingBook Learn more on our blog