The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
3 5 4 /
UFALME WA MUNGU
juu ya wanadamu kabla ya hukumu ya mwisho kutokea. Katika sura za mwisho za Ufunuo wa Yohana tunaona hukumu ya viongozi wanaokufuru, ambao wanatupwa katika ziwa la moto kwa kiberiti, hii ikiwa ni taswira yenye nguvu ya mateso, taabu, na hukumu (19:20-21). Ibilisi, ambaye anakamatwa na kutupwa katika kuzimu wakati wa kipindi cha miaka 1,000 ya amani ya milenia (20:1-3), anaachiliwa, na kusababisha udanganyifu mpya kwa mataifa. Katika tukio la kustaajabisha, mbingu na dunia zinakimbia kutoka mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, vitabu vya hukumu vinafunguliwa (mfano unaomaanisha kuhifadhiwa kwa umakini kwa matendo yote), na wale wote ambao hawapatikani katika Kitabu cha Uzima wanatupwa katika ziwa linalowaka kiberiti (20:11-15). Taswira hii ya kustaajabisha ya hukumu ya mwisho inadhihirisha upana wa upeo wa hukumu ya ulimwengu (20:11; 21:1). Kitabu kinamalizia kwa kushuka kwa Yerusalemu Mpya kama makao ya Mungu pamoja na wanadamu, mbingu mpya na nchi mpya zikishushwa, na watakatifu wa Mungu wakiishi katika uumbaji mpya ambapo Yesu ni nuru ya mji huo milele (Ufu. 21-22). Kisha yale maono makuu ya kinabii ya kale yatakuwa halisi: Bwana atafanya vitu vyote kuwa vipya katika ulimwengu wake ulioumbwa upya (Isa. 11:6-9; 65:17-25 rej. Rum. 8:22-23). Nguvu halisi ya fundisho la hukumu ya mwisho, kuhusiana na utimilifu wa Ufalme wa Mungu, ni uwezo wake wa kuhamasisha kujitoa na ufuasi wa dhati. Tukijua kwamba hivi karibuni ulimwengu utakabiliwa na jicho la hatari la Bwana wa Majeshi, wazo hili linapaswa kuzalisha ndani yetu msukumo wa maisha ya kimungu na huduma yenye ubunifu, tukijua kwamba mbingu zenyewe zitateketezwa katika ule wakati ujao wa kufanywa upya kwa vitu vyote (2 Pet. 3:11-13). Tafakuri ya Kikristo haiwezi kamwe kuzama kwenye kina cha mambo ya ajabu yanayowangoja wale wanaomwamini Yesu Kristo. Kila kitu kinachorejelea mabadiliko yanayotungoja kinaonyesha kwamba uumbaji mpya utapita yote tunayoyajua; si kwamba tutakuwa spishi mpya, bali jamii mpya ya wanadamu. Kuhusiana na ulimwengu na maisha kama tunavyoyafahamu, kutakuwa na mambo yatakayoendelea na mengine kukoma. Kwa mfano, miili yetu haitaainishwa tena kama miili ya nyama na damu (1Kor. 15:50), lakini itakuwa na aina fulani ya mwendelezo na miili yetu ya sasa, labda kwa maana zote mbili, yaani umbo na “fizikia mpya” ya miili yetu mipya (k.m.,
14 Ukurasa 126 Kipengele V
Made with FlippingBook Learn more on our blog