The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 5 3

UFALME WA MUNGU

yetu ya miungu ya uongo na mazoea ya kipagani (Isa. 2:18-20; Sef. 1:8), aina zote za jeuri ya wanadamu na ulaghai (Sef. 1:9), kutojali na uzembe wa kiroho (Sef. 1:12), na kila kitu kinachotufanya sisi kuitwa watenda-dhambi (Isa. 13:9). Siku ya Bwana ni ya ulimwengu wote katika upeo, ikishughulika na Mataifa na watu wa agano (rej. Amosi 1:2; 9:1-4; Yoeli 3:2; Mal. 3:2-5), ambao wote watasafishwa na kutakaswa ili kuondoa katika uumbaji wa Mungu vitu vyote vinavyochukiza utakatifu wake na fadhili zake. Matokeo yenye utukufu yatakuwa ni ujuzi wa Mungu kwa ulimwengu wote kati ya watu na mataifa yote, pamoja na ujuzi wa Mungu kugusa kila jamaa, lugha, kabila, na taifa (Isa. 11:9). Katika Agano Jipya, hukumu ya mwisho inaonekana katika mwanga wa Ufalme wa Mungu, na jukumu la Yesu kama Hakimu wa mwisho (2 Tim. 4:1), ambaye mwenyewe atasimamia na kutekeleza hatima na hali ya mwisho ya wanadamu wote ( Mk. 15:62; Mt. 10:15; 11:22, 24; 12:36, 43; 41). Hukumu ni wakati wa kupepeta na kutenganisha, wa kutambua yote yanayoudhi na kuyatenganisha na nchi mpya ya Mungu iliyoumbwa upya (Mt. 13:41-43, 47-50). Baba amempa Mwana jukumu la Hukumu ya Mwisho (5:26-27), na itafuatwa na ufufuo wa wenye haki na wasio haki (5:28-29 na 1 Kor. 15:22-25). Zaidi ya hayo, hali ya mwisho ya vitu vyote imeunganishwa na sifa zake: hukumu ya mwisho chini ya uangalizi wa Kristo itakuwa ya haki kabisa (Rum. 2:11), itaenea kwa watu wote kila mahali (Rum. 2:6; 14:10; 2 Kor. 5:10), na itakuwa kamilifu (Rum. 2:16). Ingawa inakawia, itakuja bila shaka (2 Pet. 2:4-10; Yuda 5-7). Ni muhimu kutambua kwamba upatanisho na kuhesabiwa haki kwa waamini vimebadilisha mwisho na ladha ya hukumu kwa Wakristo. Kwa sababu suala la dhambi limetatuliwa milele pale Kalvari (Rum. 3:21-26; 8:1, 31-34; Ebr. 10:10,14), wanafunzi wa Yesu wanahukumiwa kuhusu thawabu zao kwa ajili ya utumishi kwa Kristo (Rum. 14:10; 1 Kor. 9:24-27; Yakobo 2 Kor. 1:12; Yak. 3:13-15). Bila shaka msiba wa kutisha zaidi katika maisha yote ni ukweli kwamba, wasioamini watatengwa na uwepo na uzima wa Mungu milele kama matokeo ya hukumu na hatima yao ya mwisho, (1 Thes. 5:3; 2 Thes. 1:9; Flp. 1:28; 3:16; Rom. 1); hukumu ya Mungu ni ukweli wa sasa na ujao (Warumi 1:18-32). Kikitoa aina ya ratiba ya matukio ya jumla, kitabu cha Ufunuo kimetoa madokezo kuhusu hatima ya mwisho ya wale wanaopinga utawala wa Mungu. Kupitia hukumu za zile tarumbeta saba (8-11) na bakuli saba (16), tunaona ole na taabu zenye kutisha

Made with FlippingBook Learn more on our blog