The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 5 2 /

UFALME WA MUNGU

Maoni mbalimbali ya dhiki yote yanategemeana na yanaingiliana na mafundisho ya Biblia kuhusu “dhiki kuu,” neno linalohusishwa na nyakati za mwisho, na hasa marejeleo na mafundisho ya Yesu na Mtume Yohana. Neno kamili, “dhiki kuu” (Mt. 24:21; Ufu. 2:22; 7:14, katika Kiyunani thlipsis megale ), hudokeza kiwango cha dhiki itakayotukia wakati wa mwisho, na kwa hiyo huweza kuitofautisha na dhiki inayojulikana na inayoendelea ambayo wanafunzi wa Yesu wanaistahimili wanapoishi ulimwenguni (k.m. Yoh. 16:33). Neno hili limekuja kurejelea aina ya lugha ya mkato ya kitheolojia, muhtasari mfupi na wenye nguvu wa wakati ujao wa kutisha, wa kimataifa, na wakati wa kipekee wa machafuko ya ulimwenguni pote, hukumu, na matatizo ambayo yenyewe katika mtiririko wa kihistoria yataitangulia parousia , ufunuo mtukufu na mkuu wa Yesu Kristo kurudi duniani katika utukufu mkuu. Dhiki kuu inarejelewa katika tafsiri zinazofanana, zinazorejelea tukio lilelile kwa kutumia maneno tofauti, kama vile katika Marko 13:19 ambapo tukio hilo linatafsiriwa “dhiki,” katika Luka 21:23 ambalo linazungumzia matukio yanayohusiana na dhiki kuu kama “dhiki kuu” na katika Ufunuo 3:10 kama “saa ya kuharibiwa” ambayo itayapata mataifa yote. Kiini cha mijadala ya dhiki kinahusu asili ya ushiriki wa Kanisa katika kipindi hiki cha kutisha na kisichoweza kurudiwa cha hukumu na shida. Je, Kanisa litapitia kipindi hicho, na kuokolewa baadaye (mtazamo wa baada ya dhiki au posttribulationism ), litaokolewa kabla ya hukumu za kutisha kuanza (mtazamo wa kabla ya dhiki au pretribulationism ), au je, ukombozi wa Kanisa utatokea muda fulani katikati ya kipindi cha dhiki kuu (mtazamo wa katikati ya dhiki au midtribulationism )? Bila kujali maoni ambayo mtu anatoa, sisi tunaoamini tunamjua Mungu wetu kuwa ngome siku ya taabu (Nah. 1:7), ni Mungu anayewajua wale wanaomtumaini na anajua jinsi ya kuwaokoa walio wake kutoka katika moto na gharika (Isa. 43:1-2). Hukumu ya mwisho ni sehemu muhimu ya utimilifu wa Ufalme, na inashuhudiwa mengi, katika Agano la Kale na Jipya. Katika Agano la Kale, kwa mfano, maandiko yanaonekana kuzingatia jinsi unabii unavyoizungumzia siku ya Yahweh, wakati Mungu Mwenyezi atakaposhughulikia maovu yote ambayo kwayo wanadamu wameharibu uumbaji wake. Katika siku hiyo ya matukio mazito na ya kustaajabisha, Bwana atakomesha aina zote mbalimbali za uasi ambazo zimekuwa utambulisho wa wanadamu tangu Anguko. Hilo linatia ndani kiburi chetu (Isa. 2:12-17), ibada

 12 Ukurasa 118 Kipengele II-B

 13 Ukurasa 123 Kipengele IV

Made with FlippingBook Learn more on our blog