The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

4 4 /

UFALME WA MUNGU

Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu Sehemu ya 1

YALIYOMO

Mch. Dr. Don L. Davis

Tangu Anguko, utawala wa Mungu umezinduliwa katika ulimwengu huu wa sasa, kwanza, kama matakwa ya Mungu mwenyewe kama Shujaa juu ya adui zake, kupitia ahadi ya agano ya ukombozi aliyopewa Ibrahimu, na kupitia historia ya shughuli na kazi za Mungu pamoja na Israeli, watu wake wa agano. Kusudi letu katika sehemu hii ya kwanza ya Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu ni kukuwezesha kuona kwamba: • Tangu mwanzo, Mungu amekusudia kukomesha kutotii na uasi wote ambao ni matokeo ya Anguko. • Mungu anatenda kazi katika ulimwengu kama Shujaa dhidi ya wale wanaopinga Ufalme wake katika ulimwengu huu ulioanguka. • Kupitia agano lake na Abramu, Mungu alitoa ahadi yake ya dhati ya kumleta Mzao ambaye kupitia kwake ufalme na utawala wa shalom na haki ungerejea duniani. • Kupitia watu wa Israeli, yaani, wale wazao wa agano la Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, Mungu amefanya kazi ya kumleta Masihi, na kupitia huyo kuzindua utawala wa Mungu katika ulimwengu huu ulioanguka na uliolaaniwa kwa sababu ya dhambi.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

ukurasa 320  4

2

I. Utawala wa Mungu umezinduliwa kwa sababu Mungu Mwenyezi amekuwa Shujaa wa amani na haki katika enzi hii iliyoanguka.

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

A. Proto-evangelium : uadui kati ya nyoka na Uzao.

ukurasa 321  5

Made with FlippingBook Learn more on our blog