The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 5

UFALME WA MUNGU

Utangulizi wa Moduli

Salamu, wapendwa marafiki, katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Kati ya mambo yote yaliyohubiriwa na kufundishwa na Yesu wa Nazareti, hakuna somo lolote lililo muhimu na lenye kubishaniwa kama habari ya Ufalme wa Mungu. Wasomi wote wa kihafidhina na wasomi huru wanakubali kwamba somo alilopenda zaidi Yesu, ambalo alihubiri na kufundisha mara nyingi zaidi, ni Ufalme wa Mungu. Lilikuwa ni ujumbe wake wa wokovu, mpango wake mkuu, na theolojia yake pendwa na ya moyo wote. Cha kusikitisha ni kwamba, Kanisa la kisasa linaonekana kutozingatia sana kile ambacho Yesu alikiona kuwa muhimu zaidi katika huduma yake ya kinabii na ya Kimasihi. Tumaini letu ni kwamba moyo wako utashikwa na hadithi ya ufalme – Mfalme na Ufalme wake – na kuona umuhimu wake katika maisha ya ufuasi wa kibinafsi na huduma. Somo la kwanza, Kupingwa kwa Utawala wa Mungu , linalenga juu ya Mungu kama Mkuu na Mwenye Enzi. Somo hili linazungumzia jinsi enzi kuu na ubwana kamili wa Mungu ulivyopuuzwa na ibilisi na malaika zake, na wanadamu wawili wa kwanza, Adamu na Hawa, kupitia kutotii kwao kimakusudi katika bustani. Uasi huu ulileta matokeo ya kusikitisha ulimwenguni, katika asili ya mwanadamu, na ukasababisha kuenea kwa milki ya giza ulimwenguni. Hata hivyo, licha ya uasi wetu, Mungu anakusudia kurejesha mbingu na nchi chini ya utawala wake, na kuumba upya ulimwengu ambamo jina lake litatukuzwa, na haki na amani yake vitatawala milele. Katika somo letu la pili, Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu , tutachunguza nia ya Mungu ya kuondoa uasi na ukaidi wote ambao ni matokeo ya Anguko – Mungu anakuwa Shujaa katika ulimwengu huu ulioanguka. Mungu alifanya agano na Abramu kama ahadi yake ya dhati ya kumleta Mzao ambaye kupitia kwake ufalme na utawala wa shalom na haki ungerejea duniani. Ahadi hii ya agano ilifanywa upya kwa Isaka na Yakobo, kwa taifa la Israeli, kwa kabila la Yuda, na hatimaye kwa familia ya Daudi. Hapa tunafuatilia kwa karibu asili ya Masihi, ambaye kupitia Yeye utawala wa Mungu unarudi katika ulimwengu huu ulioanguka na uliolaaniwa kwa sababu ya dhambi. Yesu wa Nazareti ni utimilifu wa uwepo wa Ufalme, huku utawala wa Mungu ukidhihirishwa katika kuvaa kwake mwili (umwilisho), kifo, ufufuo, na kupaa kwake. Somo la tatu na la nne linahusu Uvamizi wa Utawala wa Mungu na Kukamilishwa kwa Utawala wa Mungu mtawalia. Sasa kwa kuwa Bwana wetu Yesu alikufa, akafufuka, na kupaa mbinguni, Ufalme wa Mungu unatangazwa katika ulimwengu wote na

Made with FlippingBook Learn more on our blog